32.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 20, 2024

Contact us: [email protected]

RAILA ODINGA AISIKITISHA MAREKANI

WASHINGTON, MAREKANI

SERIKALI ya Marekani imesikitishwa na hatua ya mgombea urais kwa tiketi ya Muungano wa Upinzani nchini Kenya, Nasa, Raila Odinga, kujitoa kushiriki katika uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika Oktoba 26, mwaka huu baada ya kufutwa matokeo ya urais ya uchaguzi wa Agosti 8, mwaka huu.

Taarifa ya Serikali ya nchi hiyo ilitolewa kupitia Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya na kusisitiza kuwa inaheshimu lakini inasitikishwa sana na uamuzi wa kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, kujiondoa kwenye uchaguzi mpya wa urais Oktoba 26 mwaka huu ambao angepambana tena na mgombea wa Chama cha Jubilee, Uhuru Kenyatta.

Hata hivyo, Marekani imeendelea kusisitiza kuwa itaendelea kushinikiza kuwepo kwa uchaguzi utakaokuwa huru na haki. Ofisa wa juu katika Wizara hiyo ameviambia vyombo vya habari kuwa, pamoja na hilo Odinga anakaribishwa nchini Marekani.

Taarifa hii imekuja baada ya kuwepo kwa madai kuwa Odinga amenyimwa Visa ya kwenda Marekani. Marekani imesema hakuna kinachomzuia Odinga kuja nchini Marekani wakati wowote anaotaka.

Kwa sasa Odinga yupo jijini London nchini Uingereza, anakotoa midhahara ya kisiasa na kukutana na viongozi mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles