25.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 20, 2024

Contact us: [email protected]

MAELFU YA WATU WAKOMBOLEWA SYRIA

DAMASCUS, Syria

IMERIPOTIWA kuwa hadi sasa asilimia 92 ya wananchi raia wa Syria wameshakombolewa kutoka mikononi mwa maeneo yanayoshikiliwa na wapiganaji wa  kikundi cha kigaidi cha Kiislamu nchini humo, ISIS.

Kwa mujibu wa jarida linalochapishwa kila wiki na Wizara ya Ulinzi ya Urusi, Krasnaya Zvezda, raia hao wameokolewa kutokana na msaada wa jeshi hilo tangu serikali ilipoamua kujitosa katika mgogoro huo.

Jarida hilo lilieleza kuwa katika vita hiyo vikosi vya anga vya Urusi vilifanya kazi kubwa ya  kupambana na wapigaji hao wapatao 517. Lilieleza kwamba katika mapambano hayo vilifanikiwa kuharibu zaidi ya vituo 1,260 vilivyokuwa vikimilikiwa na kundi hilo la kigaidi la kimataifa.

Lilieleza pia kwamba idadi hiyo inajumuisha zaidi vituo 139 vya kurushia makombora na vingine 129 ambavyo vilikuwa vikitumika kuwahifadhi wapiganaji wa kundi hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles