28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Raila aruka vihunzi Kenya

Raila odingaNa Mwandishi Wetu, Nairobi

MUUNGANO wa Mageuzi na Demokrasia (CORD) nchini Kenya umepata ushindi mkubwa katika mvutano unaoendelea kuhusu uhalali wa sheria wa kufanyika maandamano ya kuipinga Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).

Jaji wa Mahakama Kuu ya nchi hiyo, Joseph Onguto, alishindwa kutoa uamuzi wa kuzuia maandamano hayo ya kila wiki.

Katika maandamano hayo  wapinzani wanataka IEBC ivunjwe kwa kile wanachosema imekosa uhalali wa kusimamia uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Badala yake, Onguto alimuagiza Inspekta Jenerali wa Polisi, Joseph Boinet kuhakikisha usalama, sheria na utulivu vinadumishwa wakati wa maandamano hayo dhidi ya IEBC.

Jaji alisema viongozi wa CORD na wafuasi wao wana haki ya kuandamana kama njia ya kuwasilisha kilio chao.

Hata hivyo, aliwaonya dhidi ya kutumia nguvu kuwaondoa makamishina wa IEBC   ofisini na pia alipiga marufuku maandamano na migomo kufanyika katika maeneo binafsi.

Jaji Onguto alikuwa akitoa uamuzi wa kesi iliyofunguliwa na wabunge watano wa Muungano wa Jubilee wanaotaka viongozi wa CORD wafungwe jela kwa kuidharau mahakama.

Wabunge hao walifungua kesi dhidi ya Raila Odinga, Kalonzo Musyoka, Moses Wetangula na James Orengo wakiwatuhumu kwamba walikiuka magizo ya mahakama.

Wabunge hao walidai maandamano ya kila wiki ya CORD yalipigwa marufuku na Jaji Isaac Lenaola lakini Cord iliendelea kuyaendesha.

Jaji Lenaola aliwaonya waandamanaji wa CORD dhidi ya kuvamia   ofisi za IEBC   kuwaondoa makamishina. Pia alitoa uamuzi kuwa maandamano lazima yahakikishe sheria na utulivu vinadumishwa.

Cord kwa upande wao walisisitiza kwamba uamuzi haukuzuia kufanyika   maandamano hayo.

Orengo alisema kwamba hakuna agizo lolote linalozuia Mkenya yeyote kukutana kwa mujibu wa Ibara 37 na  38 ya Katiba ya nchi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles