28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Museveni ampa mkewe wizara nyeti

Yoweri MuseveniKAMPALA, UGANDA

RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni ameteua baraza kubwa zaidi la mawaziri, huku akimteua mkewe Janet kuwa Waziri wa Elimu na Michezo.

Wizara hiyo ni miongoni mwa zile zinazopokea fungu kubwa la bajeti na ambayo kwa miaka mingi imekuwa ikikumbwa na migogoro.

Akiingia muhula wake wa tano wa urais, Museveni mwenye umri wa miaka 71, pia amewajumuisha wapinzani katika Serikali yake.

Uamuzi wa kumteua mkewe umewashangaza wengi, huku duru za siasa zikizidi kukosoa kuhusu kushuka kwa ubora wa elimu nchini humo.

Tangu mwaka 2009, Janet alikuwa naibu waziri katika Wizara ya Masuala ya Karamoja kabla ya kuwa waziri kamili mwaka 2011.

Karamoja, jimbo lililopo kaskazini mashariki mwa Uganda, kwa muda mrefu lilikuwa eneo lililodharaulika na moja ya mambo ya kukumbuka ni pale waziri wa zamani na mpiganaji wa msituni, Tom Butiime alipokataa wadhifa wa kulitumikia kutokana na kutengewa kiwango kidogo mno cha fedha.

Wakati mke wa rais alipoanza kutumikia wadhifa wa jimbo hilo, Karamoja ilifufuka na aliiwezesha kuvutia uwekezaji na kuanza kuonekana eneo la maana machoni mwa umma.

Wanasiasa wawili muhimu wa upinzani, Betty Olive Kamya, kiongozi wa Chama cha Uganda Federal Alliance (UFA) na Betty Amongi wa Chama cha Uganda People’s Congress (UPC), ambaye pia ni mke wa Jimmy Akena, mtoto wa Rais wa zamani, Milton Obote  – nao wamo katika baraza hilo.

Kamya anakuwa Waziri wa Mamlaka ya Jiji la Kampala na Among, Waziri wa Nyumba na Ardhi.

Janet alistaafu katika siasa za uchaguzi mwaka huu akikataa kuwania tena ubunge wa Jimbo la Ruhama katika Wilaya ya Ntungamo, hivyo kujumuishwa kwake katika baraza hilo kumewashtua wengi na hilo linaweza kuashiria mipango ya Museveni kustaafu mwaka 2021.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles