30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Profesa Mbwete ataka vyuo  binafsi visifungiwe na serikali

Na PATRICIA KIMELEMETA

Aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Profesa Tolly Mbwete, ameishauri Serikali kutovifungia vyuo binafsi badala yake wavishauri ili viweze kuboresha mazingia ya utoaji wa elimu.

Kauli hiyo imekuja wiki moja baada ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), kuvifungia baadhi ya vyuo nchini kwa sababu mbalimbali ikiwamo ya kukosa vigezo.

Akizungumza na MTANZANIA Jijini Dar es Salaam jana, Profesa Mbwete ambaye kwa sasa ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kampala(KIU), kitivo cha Sayansi ya Mazingira, alisema kazi ya TCU ni kuvishauri na kuvisaidia vyuo hivyo ili viweze kuboresha mfumo mzima wa utoaji wa elimu na siyo kuvifungua.

Alisema kutokana na hali hiyo, TCU ilipaswa kukagua changamoto zilizopo na kuvishauri ili viweze kufanya marekebisho, jambo ambalo linaweza kuwasaidia wanafunzi kuendelea na masomo kama kawaida.

“TCU ilipaswa kuvishauri vyuo binafsi ili viweze kurekebisha changamoto zilizopo huku wakiendelea kudahili wanafunzi, kuliko kuvifungia hali inayosababisha wanafunzi walioomba vyuo hivyo kukosa elimu,”alisema profesa Mbwete.

Alisema Tanzania bado iko kwa iadi ya wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu, ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika.

Kutokana na hali hiyo, alisema uwepo wa vyuo binafsi ni muhimu ili viweze kusaidiana na vyuo vya serikali kwenye udahili na utoaji wa elimu, hali ambayo inaweza kupunguza ukubwa wa tatizo.

Alisema hakuna nchi duniani ambayo haina vyuo binafsi, hivyo dosari zinazojitokeza kwenye vyuo hivyo ni vema vikatatuliwa wakati wanafunzi wanaendelea na masomo yao.

“Lengo letu ni wanafunzi waweze kupata elimu bora ambayo itawasaidia mara baada ya kumaliza masomo yao, hivyo basi vyuo binafsi na serikali ni muhimu vikishindanishwa ili kuleta chachu ya elimu bora,”alisema.

Aliongeza kinachohitajika sasa hivi ni serikali kushirikiana na vyuo hivyo ili viweze kutatua changamoto zilizopo badala ya kuvifungia.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles