33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

POLISI YAMPUUZA MZEE WA UPAKO

 Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Antony Lusekelo
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Antony Lusekelo

HERIETH FAUSTINE NA JULIETH JULIUS-DAR ES SALAAM

ZIKIWA zimepita siku tatu tangu Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Antony Lusekelo, maarufu ‘Mzee wa Upako’ kusema waandishi waliomwandika vibaya watakufa kabla ya Machi mwakani, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limesema kuwa anayeamini maneno hayo ni mpagani.

Mzee wa Upako aliitoa kauli hiyo Jumapili, Desemba 11 kanisani kwake Ubungo River Side, baada ya vyombo vya habari kuandika habari ya kumfanyia fujo na kutishia kumuua jirani yake.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro, alisema watu wengine ni wapagani, hawamjui Mungu na wakisikia habari kama hizo wanaanza kuwa na wasiwasi.

“Kuhusu taarifa ya Mchungaji Lusekelo nilishajibu toka jana (juzi) na magazeti yaliandika, watu wengi ni wapagani, hawamjui Mungu, wakisikia habari kama hizo wanaanza kuwa na wasiwasi kutokana na upagani wao, lakini Mungu ni mmoja, ndiye aliyekuleta duniani na ndiye atakayekutoa, mtu hupwasi kuogopa maneno kama hayo,” alisema Kamanda Sirro.

Taarifa za vitisho hivyo kwa waandishi wa habari, zinaweza kunasibishwa na kauli zilizowahi kutolewa kwa nyakati tofauti na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alitoa kauli za kichochezi dhidi ya  Rais Dk. John Magufuli.

Akiwa katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Baraa jijini Arusha, Lema alisema “kama Rais Magufuli akiendelea na kiburi cha kujiona yeye ni Mungu, basi Mungu atachukua maisha yake kabla ya kufika 2020”.

Akizungumza kanisani kwake, Mchungaji Lusekelo alisema kila aliyeshiriki kumchafua, wakiwamo waandishi wa habari, ikifika mwezi wa tatu wakiwa hai ataacha kazi ya kuhubiri na kwenda kuuza gongo.

“Kila mwandishi aliyeniandika vibaya, ikifika mwezi wa tatu akiwa hai, mimi naacha kuhubiri, nafunga virago nakwenda kuuza gongo, sasa Mungu ndiye ataamua kwamba niache kuhubiri au wewe ufe,” alisema Mchungaji Lusekelo.

Novemba 25, mwaka huu, mchungaji huyo alidaiwa kufanya vurugu kwa majirani zake, huku video aliyorekodiwa eneo la tukio, ikimwonyesha akiongea kama mtu aliyelewa chakari.

Mwishoo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles