24.7 C
Dar es Salaam
Saturday, April 13, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI YATANGAZA AJIRA WALIMU WA SAYANSI

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Maimuna Tarishi.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Maimuna Tarishi.

Na PATRICIA KIMELEMETA – dar es salaam

SERIKALI imetangaza ajira kwa walimu wa masomo ya sayansi na hisabati waliomaliza kozi ya shahada na stashahada na kuhitimu mwaka 2015.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Maimuna Tarishi, wahitimu hao wanatakiwa kuwasilisha  nakala za vyeti  vyao kwa elimu ya sekondari kidato cha nne na sita na taaluma ya ualimu wa shahada na stashahada kwa uhakiki.

Alisema waombaji wanatakiwa kuwasilisha nakala zao kupitia barua pepe [email protected], kuanzia tarehe ya tangazo hadi Desemba 16 ili waweze kuhakikiwa, na kwamba watakaoshindwa kufanya hivyo hawatafikiriwa katika ajira.

Tarishi alisema waombaji ambao watahitaji taarifa zaidi, wanapaswa kuingia kwenye tovuti ya Ofisi ya Rais, Tamisemi, NECTA, TCU na NACTE.

Hivi karibuni, Serikali ilitangaza kusitisha ajira zote, kama njia ya kukabiliana na wimbi la watumishi hewa, huku uamuzi huo ukienda sambamba na kusimamisha nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa Serikali na wakala zake na utoaji likizo bila ya malipo.

 UTEUZI

Wakati huo huo, Rais Dk. John Magufuli amemteua Ngusa Samike kuwa mnikulu Ofisi ya Rais, Ikulu. Awali alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli pia amemteua, Dk. Khatib Kizungu kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Dotto James aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa, ilisema kabla ya uteuzi huo, Dk Kazungu alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles