24.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

MKURUGENZI JAMII FORUMS MBARONI

Mtandao wa Jamii Forums (JF), Maxence Melo
Mtandao wa Jamii Forums (JF), Maxence Melo

Na WAANDISHI WETU – DAR ES SALAAM 

MKURUGENZI Mtendaji na mmoja wa waasisi wa Mtandao wa Jamii Forums (JF), Maxence Melo, amekamatwa na kushikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam kwa kosa la kuzuia upelelezi wa makosa ya mtandao.

Akizungumza jana kwa simu kuthibisha kukamatwa kwake, Mhariri na mwanaharakati wa kutetea uhuru wa mawasiliano, Simon Mkina, alisema Melo alifika polisi saa 6:17 mchana, baadaye saa 7 mchana aliamuriwa kuingia selo, huku waliomsindikiza wakielezwa kuondoka eneo la polisi.

Alisema Melo anakabiliwa na mashtaka ya kuzuia upelelezi wa makosa ya mtandao kwa kushindwa kutoa taarifa binafsi za watumiaji wa mtandao wa JamiiForums ambazo polisi walizihitaji.

“Maxence (Melo) alifika kituoni hapo kuitikia wito wa polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, lakini alipofika Kituo Kikuu cha Kati cha Polisi, alizuiliwa na polisi, amenyimwa dhamana ya polisi kwa madai ya kuwapo amri kutoka kwa wakubwa,” alisema Mkina akimkariri mmoja wa maofisa wa polisi aliyewajibu.

Mkina alisema hata baada ya kuwasiliana na mwanasheria wa Melo, Nakazael Tenga na kushughulikia dhamana yake, ilishindikana kwa maelezo kuwa alipaswa kulala kituoni hapo hadi kesho.

“Hata Mwanasheria Tenga alishangazwa na hatua hiyo ya Jeshi la Polisi kumnyima dhamana mtuhumiwa na kueleza kuwa alikuwa na haki ya dhamana,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles