30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

NMB yaitambia CRDB ‘Bankers Basketball League’

MICHUANO ya Mabenki kwa Mpira wa Kikapu (Bankers Basketball League – BBL 2018), imezidi kushika kasi ambapo mwishoni mwa wiki kikosi cha Benki ya NMB kiliigaragaza timu ya CRDB kwa jumla ya vikapu 52-42.

NMB chini ya kocha mkuu, Evarist Mapunda, ilitawala kwa kiasi kikubwa pambano hilo lililofanyika kwenye viwanja vya Gymkhana, jijini Dar es Salaam, ambapo walimaliza nusu ya kwanza ya mtifuano huo wakiwa mbele kwa vikapu 26-15.

Katika nusu ya pili, kujiamini kulikopitiliza kuliwafanya nyota wa NMB kupunguza kasi, ambapo walijikuta wakiimaliza nusu hiyo kwa kipigo cha vikapu 27-26, ingawa havikutosha kuwapa CRDB ushindi wa jumla, hivyo NMB kushinda 52-42.

Akizungumza baada ya mchezo, Mapunda aliwapongeza nyota wake kwa upambanaji uliofanikisha kuibuka na ushindi huo na kwamba wamejipanga kuhakikisha wanautwaa ubingwa wa michuano hiyo inayofanyika kila mwaka.

“Tumetimiza lengo la kuibuka na ushindi katika mechi dhidi ya CRDB, nawapongeza nyota wangu kwa upambanaji na sasa tunaelekea kwenye mazoezi kujiandaa na mechi zijazo kulingana na ratiba, ili kufanikisha lengo kuu la kutwaa ubingwa,” alisema Mapunda.

Kabla ya NMB kuichachafya CRDB, pambano la awali juzi lilizikutanisha DTB na TADB, ambako kikosi cha DTB kiliibuka na ushindi wa vikapu 73-40, ambako washindi waliongoza kwa vikapu 40-16 katika nusu ya kwanza, kisha 33-24 katika nusu ya pili.

Mbali na mpira wa kikapu, pia NMB iliwafunga timu ya miguu ya CRDB kwa magoli matatu kwa sifuri, mpira uliochezwa mapema na kufuatiwa na mpira wa mikono.

Bankers Basketball League 2018 ilianza kutimua vumbi Oktoba 27 mwaka huu katika viwanja vya Gymkhana, Ocean Road, jijini Dar es Salaam, ikishirikisha benki mbalimbali nchini zikiongozwa na NMB.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles