28.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

Sammata ang’ang’aniwa Ubelgiji

Na MOHAMED KASARA-DAR ES SALAAM

KIKOSI cha KR Genk anachokichezea mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta, kimelazimishwa sare ya bao 1-1 na Club Brugge katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A, uliochezwa Uwanja wa Luminuz Arena nchini Ubelgiji.

Katika mchezo huo, Samatta alicheza kwa dakika zote 90.

Genk iliandika bao la kuongoza dakika ya 10 kupitia kwa  mshambuliaji raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Dieumerci N’Dongala, lakini Siebe Schrijvers aliisawazishia Brugge dakika ya 53.
Sammata sasa amefikisha michezo 127 katika mashindano yote tangu alipojiunga na Genk, Januari mwaka 2016, akitokea TP Mazembe ya DRC.

Akiwa na Genk, Samatta tayari amefunga jumla ya mabao 51.

Katika ligi ya Ubelgiji amecheza mechi 99 na kufunga mabao 36, Kombe la Ubelgiji mechi nane, mabao mawili na Europa League mechi 20, mabao 14.
Genk inaongoza katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa imejikusanyia pointi 34 baada ya sare ya jana dhidi ya Brugge.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,085FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles