31.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

MSD mbioni kukamilisha kiwanda cha mipira ya mikono cha Idodi

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

KATIKA kufanikisha ongezeko la uzalishaji wa bidhaa za afya nchini na kuendana na azma ya Serikali ya uanzishaji wa viwanda, Bohari Kuu ya Dawa (MSD) ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha miundombinu ya kiwanda cha mipira ya mikono kilichopo Idofi mkoani Njombe.

Hayo yameelezwa Agosti 7,2023 na Meneja Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini wa MSD, Hassan Ally Ibrahim wakati akiwasilisha kwa Waandishi wa Habari, taarifa ya bohari hiyo kwa mwaka wa fedha 2023-2023 pamoja na mwelekeo wake.

Meneja huyo amesema kiwanda hicho kinatarajiwa kuzalisha takribani jozi 86,400,000 za mipira ya mikono kwa mwaka.

“Na kitachagiza uzalishaji wa malighafi ya mpira kutoka maeneo tofauti nchini,”amesema Meneja huyo.

Amesema uzalishaji huo utapunguza utegemezi wa bidhaa hiyo kutoka nje ya nchi na kuokoa matumizi ya fedha za kigeni kiasi cha Sh bilioni 33 kwa mwaka.

Aidha kiwanda hicho kitatoa ajira za moja kwa moja kwa Watanzania takribani 200.

Pia amesema Serikali kupitia Bohari ya Dawa imeongeza mtambo mwingine wa kisasa wa kuzalisha barakoa maalum aina ya N95 zenye uwezo wa kuzuia maambukizi hatarishi ya njia ya hewa na chembe chembe za vumbi la viwandani na kwenye migodi.

Amesema Kiwanda hicho kimeongezwa eneo la la Keko Mwanga, Dar es salaam ambapo kipo kiwanda kingine cha kutengeneza barakoa za kawaida (surgical mask).

“Viwanda hivi viwili vya barakoa vina uwezo wa kuzalisha barakoa milioni 10.8 kwa mwaka” amesema Meneja huyo.

Amesema utekelezaji wa majukumu haya ya Bohari ya Dawa unaenda sambasamba na utekelezaji wa maelekezo ya maboresho ya utendaji yaliyotolewa mwezi Machi 2022 na Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Hivyo, Bohari ya Dawa inapitia mifumo yote ya utendaji na uendeshaji ikiwamo maboresho ya mnyororo wa ugavi, usimamizi wa utendaji na mifumo ya TEHAMA…

“Ili kuendana na kasi ya ongezeko la ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za afya vinavyojengwa na Serikali ya awamu ya sita na kuhakikisha malengo ya Serikali katika upatikanaji wa bidhaa za afya yanafikiwa,” amesema Meneja huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles