26.7 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Juhudi za Rais Samia zimetuongezea nguvu – Dk. Abbasi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Serikali imesema iko tayari kuliwakilisha Bara la Afrika kwenye vyombo vya juu katika ngazi ya Umoja wa Mataifa katika sekta ya utalii kutokana na dhima ambayo Tanzania imepewa na Bara la Afrika katika Mkutano wa Utalii Kanda ya Afrika uliomalizika hivi karibuni nchini Maritius.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kueleza mafanikio ya Mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Hassan Abbasi, amesema kufuatia Tanzania kuchaguliwa kuliwakilisha Bara la Afrika katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UNWTO) na nafasi ya ujumbe katika Kamati ya Utendaji ya Shirika hilo, Tanzania inajipanga kuzitumikia vyema nafasi hizo.

“Tangu tuliporejea tumefikisha rasmi taarifa hizi kwa Mhe Waziri wetu, Mohamed Mchengerwa na yuko tayari kuanza kuiwakilisha nchi na Bara la Afrika katika nafasi hizo muhimu alizoteuliwa,” alisema Dk. Abbasi akiambatana na watendaji walioshiriki pia Mkutano huo wa Mauritius wa UNWTO Kanda ya Afrika ambapo ujumbe wa Tanzania uliongezwa na Naibu Waziri Mhe. Mary Masanja.

Kwa upande wao Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Utalii (TTB), Damasi Mfugale na Kaimu Mkurugenzi wa Utalii Wizarani Dk. Theresa Mugobi, walioshiriki pia Mkutano huo wamesema wamejifunza mambo mengi ikiwemo namna nchi zinavyopigania maslahi yao katika mikutano ya kimataifa na kubadilishana ujuzi katika kuendeleza na kutangaza utalii.

Akieleza zaidi siri ya mafanikio ya Mkutano huo, Dk. Abbasi amesema Wizara hiyo kwa sasa itakuwa makini zaidi kuchangamkia fursa za kimataifa kwani wamepata pia ujasiri kutokana na maono ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, aliyeshiriki filamu ya “Tanzania; The Royal Tour” kuitangaza nchi kimataifa zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles