31.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mpango maalumu wa kukusanya maziwa kuanzishwa

MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

KITUO cha Kuendeleza Kilimo Endelevu cha Sustainable Agriculture Tanzania (SAT), kilichopo mkoani Morogoro  kinatarajia kuanzisha  mpango  maalumu wa kukusanya maziwa kisha kuyachakata na kuyauza ili kuongeza idadi ya wanywaji wa maziwa na kipato kwa wafugaji nchini.

Akizungumza na MTANZANIA mwishoni mwa wiki Ofisa kutoka SAT, Kashingye Salum alisema unywaji maziwa unatishia usalama wa afya za wananchi wengi kwakuwa kiwango cha mtu mmoja kunywa maziwa kwa mwaka ni lita 400 lakini wengi wana wastani wa lita 47 kwa mwaka jambo ambalo ni hatari kiafya na jitihada za haraka zinatakiwa kuchukuliwa ili kuongeza lita za unywaji kwa mwaka.

Salum alisema  Serikali imeweka mikakati kadhaa kuhakikisha unywaji maziwa unafikia angalau kiwango cha lita 200 kwa mwaka na ndio maana imepandisha hata kodi za maziwa yanayotoka nje ya nchi ili kuchochewa soko la ndani.

“Zamani ukileta maziwa kilogramu moja unatozwa Sh.150 lakini ili kukuza uchumi wa ndani sasa hivi kodi imepanda kwa kilogramu moja unalipa shilingi 2,000 na sisi kama SAT tumeona ni fursa mwaka huu tufunge kituo maalum cha maziwa litaongeza idadi ya wanywaji na kipato pia,” alisema Salum.

Alisema Tanzania ina mifugo mingi lakini uzalishaji wake ni mdogo na ndio maana SAT kwa kushirikiana na Chuo cha Kilimo Sokoine (SUA), mikakati na tafiti mbalimbali ili kuwaendeleza wakulima na wafugaji.

Alisema walifanya utafiti na kubain idadi ya maziwa yanayopatikana katika eneo la wafugaji wa Morogoro wastani kwa siku uzalishaji ukiwa mkubwa ni lita zaidi ya 300 na ukiwa mdogo ni lita 119.

Salum alisema wengi walielezea kuwa maziwa hayo huuzwa kiasi cha Sh 500 hadi 600 kwa lita wakati thamani halisi ni Sh 900.

“Tuliamua kupanga mikakati kadhaa ambayo kwa kiasi fulani imesaidia kuwaongezea kipato wafugaji ambapo lita 8,000 kwa siku na hadi sasa wameanza kupata lita 4,000,” alisema

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa SAT, Janeth Maro alisema, mradi huo ambao utakamilika mwaka huu utatekelezwa katika kijiji cha Mangae kata ya Kubuni Morogoro Vijijini.

Alisema awali walibaini ng’ombe waliokuwa wanafugwa katika kituo hicho hawana uwezo wa kuzalisha maziwa mengi kwakuwa walikuwa wanatoa lita moja kwa siku hivyo wakaamua kubuni mbinu nyingine ili kuongeza idadi ya maziwa na nyama bora.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles