24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Shaka: Upinzani hautaizua CCM kurudi Ikulu

MWANDISHI WETU-MOROGORO

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM ), Mkoa Morogoro kimesema ufanisi wa kazi za maendeleo uliopatikana ikiwemo serikali kusimamia nidhamu ya kazi kupitia utekelezaji ilani ya uchaguzi ya CCM chini ya serikali ya Awamu ya Tano upinzani hautafurukuta wala wananchi hawawezi fikiria tena ndoto za kuwapata ridhaa ya uongozi kuiongoza dola ya Tanzania

Hayo yalisemwa jana na Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro, Shaka Hamdu Shaka,  alipokuwa akizungumza na wananchi na wanachama wa Kata Ruaha Wilaya ya Kilosa mkoani hapa mara baada kuwapokea madiwani wa Chadema waliojiunga na CCM.

Alisema upinzani kushinda uchaguzi na kutarajia kuwaongoza wananchi milioni 55 si kazi rahisi kama baadhi ya vyama na viongozi wake vinavyojiaminisha huku baadhi ya wanasiasa waliodhani Chadema  pamoja na vyama vingine vikishuhudia vigogo wake wakihama na kujiunga na CCM ni dalili tosha kwamba vyama hivyo vimekosa mwelekeo na matumani kwa Watanzania.

Alisema wananchi ni werevu ,wana upendo na maarifa ya kupambanua mambo huku wakijua aina ipi ya viongozi wanaowafaa na kuwategemea katika medani za uongozi, utawala na chama chenye sera bora na siasa safi.

“Kuongoza serikali si kazi kama kucheza mdundiko au ifanane na maabara inachofanyiwa majaribio ya chanjo, dawa na tiba. Kuongoza nchi ni kazi nzito inayohitaji uzoefu, umakini na uthubutu, mtu yeyote ni rahisi kutamani urais lakini kuitendea haki nafasi hiyo ni mtihani kabambe,” alisema Shaka

Katibu huyo wa CCM alisema kwamba kuna uguku katika kuongoza dola hasa kwa nchi za Bara la Afrika kwani suala hilo ni sawa na kazi ya kujitolea muhanga kufa na kupona na kiongozi ni lazima akubali kuongoza kwa haki, kuleta mageuzi yenye tija na manufaa.

Pamoja na hili alisema kuwa pia kiongozi lazima akuze uchumi , kusimamia matumizi bora ya rasilimali zilizopo , pia akitakiwa avae miwani ya mbao na kufumba macho saa 24.

Alisema kuwa jukumu la kusimamia haki na wajibu kwa wananchi milioni 55 si nyepesi kama inavyofikiriwa na baadhi ya vyama kwani Rais anahitaji awe na misuli ya kulinda rasimali, kupambana na udhirifu wa mali za umma , awakabili vibaraka walioghilibiwa kwa pipi huku akisimamia umoja ma amani.

“Kazi iliofanywa na Rais John Pombe Joseph Magufuli kwa miaka minne si kazi lelemama. Ni ya kukata na shoka imetoa jasho jingi mwilini. Kazi ya kumsulubu nyani anayefanana na binadamu ni ngumu . Kumtazama nyani usoni, akilia na kutoa machozi ili umoenee huruma inahitaji ujasiri,” alisema

Aidha Katibu huyo aliwataka wananchi mkoani Morogoro kuendelea kumuunga mkono Rais Dk. Magufuli kutokana na nia yake safi na ya kizalendo jinsi anavyowatetea masikini na wanyonge , akipambana , kukomesha ufisadi na rushwa , huku serikali yake ikikusanya kodi na huduma za jamii zikimarika.

“Kuongoza serikali Barani Afrika lazima uwe tayari kuhimili mikiki na vishindo vya wanyonyaji ili wasiidhoofishe maendeleo. Wakati ukitimiza wajibu huo , maadui zako wanakupiga vita bila sababu zozote .

“Ukitazama nyuma yao wapo kina nani utawakuta walafi madaraka wamejificha. Ikiwa huna afya ya uzalendo watakuyumbisha,” alisema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles