32.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 20, 2024

Contact us: [email protected]

MOI kutoa huduma kwa viwango vya kimataifa

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) imesema itaendelea kuboresha huduma zake ili kuendana na zile zinazotolewa nje ya nchi ikiwamo Ulaya na Indialengo likiwa ni kufungua milango kwa wateja wa nje ya nchi.

Hayo yamebainishwa na Oktoba 8, jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Upasuaji wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu, Dk. Laurent Mchome alipotembelea maonyesho ya saba ya Site Swahili International Tourlism Expo ambapo amesema kuwa wanaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kupanua huduma ya tiba ndani na nje ya nchi.

Amesema ili kuendana na sera ya Tiba Utalii, walifungua tawi la huduma hiyo kwa ajili ya wagonjwa wa nje ya nchi na Watanzania wanaotaka kutumia huduma hiyo.

“MOI tuna huduma nyingi za kibobevu ikiwemo za vifaa bandia ikiwemo mikono na miguu bandia kwa sasa tuna mikono bandia ambayo ni smart unaweza kufanyia kazi mkono wa bandia kunyanyua maji kushika chochote, yote hiyo ni kuhakikisha wanatatua huduma zao na kuweka ngazi ya kimataifa,” amesema Dk. Mchome.

Amesema wanafanya upasuaji wote wa ubongo, mgongo, mifupa pamoja na viungo wamekuwa wakifanya kwa mda mrefu kikiwa ndio kituo kwa Afrika Mashariki na Kati.

Amesema wameendeleza huduma hizo kwa kiwango kikubwa sasa hivi wanafanya huduma ambazo hawapasui kwa kiwango kikubwa kama zamani, badala yake sasahivi wanapasua kwa kiwango kidogo kuweka matundu.

Ameeleza kuwa upasuaji huo wanafanya kwenye magoti, nyonga kiwiko cha mikono na kwenye mabega.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles