22.9 C
Dar es Salaam
Monday, September 9, 2024

Contact us: [email protected]

TANAPA yatumia maonyesho ya SITE kutoa elimu kwa wadau

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limetumia Maonyesho ya Site ya Swahili Internation Tourism Expo kutoa elimu kwa wadau wa ndani na nje ya nchi kuhusu uwekezaji na mambo mengine katika hifadhi na kutatua changamoto zao.

Akizumgumza na Mtanzania Digital Oktoba 8, jijini Dar es Salaam, Mhifadhi Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo ya Biashara TANAPA, Augustine Massesa amesema lengo kubwa ni kutangaza vivutio na uwekezaji.

Maonyesho haya yanafaida kubwa kwetu kwanza kupata fursa ya kuonana na wadau wakiwamo wapya na kutoa fursa kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi kubadilisha ujuzi na mawazo,” amesema Massesa.

Amesema kutokana na juhudi zinazofanywa na Serikali katika sekta ya utalii zimechochea fursa nyingi za utalii kuongezeka.

Aidha, amesema kuna changamoto ya miundombinu lakini Serikali inaendelea kutoa fedha kwa ajili kurekebisha miundombinu.

“Jukumu la TANAPA kushirikiana na Serikali kuhakikisha tunaboresha miundombinu, huduma na miundombinu ikiwa vizuri na gharama zitakuwa nafuu na watalii kuongezeka,” amesema.

Amesema mikakati yao katika maonyesho lijalo wanatarajia wataboresha huduma zaidi na kuja na vitu vipya.

Naye Askari Uhifadhi na Muhifadhini TANAPA, Paulina Mkama amesema wanaendelea kutoa elimu kwa wadau kuwekeza katika hifadhi ikiwemo hoteli za nyota tano.

“Kuna baadhi ya wadau wameweza kupata elimu na kuweza kulipia maeneo ya kuwekeza na kuja kwenye onesho hili kuna punguza gharama na kuweza kutatuliwa changamoto hapo hapo,” amesema Paulina.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles