31.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

MKUTANO WA TRUMP, KIM SHAKAANI

WASHIONGTON, MAREKANI


RAIS wa Marekani, Donald Trump ametilia shaka uwezekano wa kufanyika kwa mkutano adimu na wa kihistoria na Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un nchini Singapore, Juni 12, mwaka huu.

Trump amekaririwa na vyombo vya habari akieleza kuwa Korea Kaskazini inapaswa kutimiza vigezo vilivyowekwa ambayo ni nadra kutokea ili mkutano ufanikiwe.

Korea Kaskazini ilikwisha toa msimamo kuwa inaweza kujiondoa katika mkutano huo iwapo Marekani itasisitiza suala la kuachana na mpango wa silaha za nyuklia.

Rais Trump alizungumzia mkutano huo mara baada ya kumpokea katika Ikulu ya Marekani, Rais wa Korea Kusini, Moon Jae-in.

Hata hivyo, Rais Trump hakuweka wazi ni masharti gani ambayo yamewekwa kwa ajili ya mkutano huo na alipoulizwa na wanahabari juu ya hilo, alisema suala la kuachana na silaha za nyuklia ni lazima litekelezwe na Korea Kaskazini.

Mkutano huo kati ya Rais Trump na Kim Jon-un unatarajiwa kufanyika Juni 12 nchini Singapore baada ya kutanguliwa na mkutano wa marais wa Korea mbili mwezi uliopita.

Trump aliongeza kuwa mwelekeo wa Kim Jong-un umebadilika baada ya ziara yake ya pili mwezi huu, nchini China.

Hata hivyo, mapema juzi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo alieleza matumaini yake kuhusu kuwepo kwa mkutano huo aliposema wanaendelea vyema na maandalizi.

Pia aliipongeza China kwa kuweka msukumo wa kihistoria kwa Korea Kaskazini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles