23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

WAZIRI AWATAKA WAISLAMU WACHUKUE LIKIZO MFUNGO WA RAMADHAN

COPENHAGEN, DENMARK


PENDEKEZO la Waziri wa Uhamiaji wa Denmark, Inger Stojberg linalowataka Waislamu kuchukua likizo wakati wa mwezi wa Ramadhani kwa ajili ya usalama wa jamii nzima limeshutumiwa vikali na Waislamu nchini humo.

Stojberg, ambaye amekuwa akifahamika kwa kutekeleza sera kali za uhamiaji, amekaririwa na vyombo vya habari vya nchi hiyo akieleza kuwa kufunga saa za kazi siku nzima kunaleta changamoto kikazi.

Kwamba kunaweza kusababisha hatari hasa kwa waendesha mabasi ya abiria na wafanyakazi wa hospitalini kufanya kazi muda mrefu bila kula.

Kampuni za mabasi zilikuwa za kwanza kusema kuwa hazina shida na Waislamu kuendelea na kazi wakati wa mwezi wa Ramadhani.

Kampuni ya mabasi ya Ariva, inayofanya safari zake nchini Denmark, imesema hawajawahi kupata ajali iliyowahusisha madereva waliofunga.

”Suala hilo si tatizo kwetu” alisema msemaji wa Ariva, Hammershoy Splittorff alipozungumza na gazeti la Berlingske Tidende.

Umoja wa Waislamu nchini hapa ulimshutumu waziri huyo na kumweleza kuwa Waislamu ni watu wazima ambao wanaweza kujichunga wenyewe na jamii kwa ujumla hata kama wakifunga.

Stojberg aliandika mawazo yake kuwa Denmark ina uhuru wa kuabudu na kuwa dini ni suala binafsi.

Lakini aliwataka Waislamu wanaofunga Ramadhani kutofanya kazi kwa kuwa wakati mwingine wanahitajika kwa saa nyingi, kazi ambazo zinahusisha pia kushika mashine hatari.

Alitoa mfano wa madereva wa mabasi ambao hawali wala kula kwa zaidi ya saa 10 na kusema kuwa kufunga kunaweza kuathiri usalama na uwezo wao wa uzalishaji

”Natoa wito kwa Waislamu kuchukua likizo wakati wa mwezi wa Ramadhani kuepuka madhara kwa jamii nzima ya Denmark,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles