25.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

MKURUGENZI BAGA AIZULIA JAMBO BANDARI

bandari

NA TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya Baga Investment imeshindwa kulipa kwa wakati posho za baadhi ya wafanyakazi wake kwa madai ya kuidai Mamlaka ya Bandari Tanzani(TPA) Sh bilioni mbili.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Jumbe Moshi, aliyasema hayo jana baada ya kuwapo kwa malalamiko ya baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo ambao wanalipwa kwa siku kudai kutolipwa posho zao kwa siku 23.

Alisema ni zaidi ya miezi mitatu sasa TPA imeshindwa kuwalipa fedha hizo hivyo kushindwa kulipa madeni yanayowakabili yakiwamo ya benki.

“Kuchelewa kulipwa kwa wafanyakazi wetu kunatokana na TPA kushindwa kuilipa kampuni kwa miezi mitatu, jambo ambalo linarudisha nyuma utendaji wa kampuni.

“Hali hii imetuweka katika wakati mgumu kutokana na kampuni kudaiwa na baadhi ya benki, hali inayofanya tushindwe kulipa na kujiendesha,” alisema Moshi.

Awali baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni hiyo ya Baga Investment, walidai kuwa hawajalipwa posho hizo kwa siku 23 sasa.

Mmoja wa wafanyakazi hao ambaye hakutaka kuandikwa gazetini, alisema kila walipouliza walijibiwa kwamba chimbuko la kuchelewa huko kumesababishwa na TPA  ambayo haijailipa kampuni hiyo kwa zaidi ya miezi mitatu.

Akizungumzia malalamiko hayo, Msemaji wa Bandari, Janet Ruzangi, alisema madai hayo hayana ukweli kwa sababu kampuni hiyo inalipwa kwa wiki.

“Sijui mkataba wao na TPA unasemaje lakini mara nyingi malipo yao yanakuwa kwa wiki au mwezi kwa sababu Baga Investment mpaka wameingia mkataba na kuendesha shughuli hiyo ina maana walikuwa wanazo fedha za kutosha na si mpaka walipwe,” alisema Ruzangi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles