Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM |
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amesema baadhi ya mbwa wa Jeshi la Polisi walioko katika Bandari ya Dar es Salaam, wanakodishwa kwa makampuni binafsi Dar es Salaam na nje ya jiji hilo.
Aliyasema hayo jana alipozungumza na MTANZANIA kwa simu baada ya ziara yake katika Bandari ya Dar es Salaam aliyoifanya kujua utendaji kazi wa bandari hiyo.
“Baada ya kufanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam leo (jana), kuna maagizo niliyatoa kutokana na taarifa nilizonazo kuhusu mbwa wa polisi.
“Taarifa nilizokuwa nazo ni kwamba pale bandarini kulikuwa na daftari lililokuwa na mbwa 23 hadi kufikia Julai 16, mwaka huu.
“Lakini, katika mazingira ya kutatanisha, Julai 17, mwaka huu lile daftari lililokuwa na idadi hiyo ya mbwa liliachwa na wahusika wakaanzisha daftari jingine jipya ambalo linaonekana kuna mbwa 60.
“Katika utafiti wangu nimegundua wale mbwa baadhi yao wanakodishwa kwa watu binafsi na wengine kwenye makampuni binafsi wakati mbwa hao ni mali ya Serikali na wanatambulika kwa majina na wanalipwa posho za kuwatunza.
“Kibaya zaidi ni kwamba …
Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.
Hiyo mbwa ikipatikana watu waliopotea nao watafutwe