28.4 C
Dar es Salaam
Friday, February 23, 2024

Contact us: [email protected]

SIMBA WAMPA MWAKA MMOJA KOCHA MBELGIJI

 NA LULU RINGO


Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba SC leo wamemtambulisha kocha mpya kutoka nchini Ubelgiji Patrick Aussems.

Utambulisho huo wa mkataba wa mwaka mmoja baina ya Simba Sc na kocha huyo umefanyika mbele ya waandishi wa habari kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar Es Salaam.

Kocha huyo kwa nyakati tofauti amewahi kuzinoa Al Hilal ya Sudan na kuibuka bingwa ligi nchini humo pia amefanikiwa kuifikisha timu hiyo hatua ya nusu fainali ya klabu bingwa Afrika.

Mwaka 2014 ameshinda ubingwa wa ligi ya Congo na kuifikisha timu hiyo hatua ya nusu fainali kombe la Shirikisho Afrika.

Licha ya kufundisha timu nyingi za Afrika amewahi pia kufundisha vikosi mbalimbali nje ya bara la Afrika ikiwemo ligi ya Ufaransa.

Sifa zote hizo ndizo zilizoshawishi uongozi wa kikosi cha Simba SC kuingia mkataba wa mwaka mmoja na kocha huyo kwa maandalizi ya Ligi Kuu na kimataifa.

Kocha huyo aliwaambia waandishi wa habari kwamba falsafa yake kwenye mchezo wa soka ni kutawala mchezo mwanzo hadi mwisho na kuhakikisha mashabiki wanakuwa na furaha muda wote.

“Kila kocha ana falsafa zake hivyo falsafa yangu ni kuhakikisha wachezaji wangu wanatawala mchezo mwanzo hadi mwisho na kuwapa mashabiki wa simba furaha, nahitaji kuona Simba wanachukua ubingwa wa ligi kuu kwa mara nyingine na kuwa mabingwa wa Afrika” alisema Kocha Patrick

Licha ya muda mfupi aliofika katika klabu ya Simba Kocha Patrick ameonekana kuwajua baadhi ya wachezaji na kusema amekuwa akiwafutilia hasa walipokuwa kwenye kombe la Kagame.

“Nimekuwa nikiifuatilia klabu ya Simba katika video nyingi hivyo nawafahamu wachezaji ninaokwenda kuwafundisha kuna Kapombe, Mlipili, Okwi, Boko, Kichuya na wengine wengi” aliwataja Kocha Patrick.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles