26 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

Martin Kadinda, Binti Salha Foundation waja na kampeni ya kusaidia wanafunzi wa kike

BEATRICE KAIZA

Mbunifu wa Mitindo nchini, Martin Kadinda akishirikiana na Binti Salha Foundation wameanzisha kampeni waliyoipa jina la ‘Mvalishe akasome’ ambayo lengo lake ni kusaidia wanafunzi wa kike wa shule za msingi na sekondari wenye uhitaji wa sare za shule.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Agosti 13, Kadinda amesema kuwa wamekabidhi sare za shule kwa wanafunzi sita katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, wanafunzi watatu wa shule za msingi na watatu wa shule za sekondari.

“Ikiwa ni sehemu ya programu yetu ya ‘Supporting Her Education katika kuhakikisha watoto wa kike wanapata elimu bora ili kuweza kufikia malengo ya maendeleo ya taifa na malengo ya maendeleo endelevu ya dunia yaani SDGs ifikapo mwaka 2030 ambapo elimu bora ni lengo namba nne.


“Mvalishe akasome ni kampeni inayolenga kupunguza wimbi la watoto wa kike wanaoshindwa kwenda shule na wanaoshindwa kumaliza shule za msingi na sekondari kwa sababu mbalimbali ikiwemo suala la kukosa sare za shule ili kuwasitiri na kuwapa hamasa ya kusoma pasipo kuangukia katika vishawishi kama mahusiano ya kimapenzi kwa nia ya kupata msaada wa fedha,” amesema Kadinda.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Binti Salha Foundation, Salha Aziz, amesema kuwa kampeni inalenga kuwafikia wanafunzi 500 wa mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Dodoma na kwamba watajikita hasa katika ukusanyaji wa sare za shule zilizokwishavaliwa lakini zipo kwenye hali nzuri ambazo wataziweka katika hali ya usafi na ubora ili kuwafikia wanafunzi wenye mahitaji ya sare za shule.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles