Marais wastaafu wa kijiji cha Maisha Plus wamelipwa fedha za kiinua mgongo kutokana na kuongoza katika kijiji hicho.
Akizungumzia zoezi hilo, Babu Rajabu alisema uongozi wa kijiji umeweka utaratibu wa kuwalipa marais wanaoongoza kijiji hicho mara baada ya kumaliza muda wao wa uongozi.
Alisema kila Rais amelipwa shilingi 200,000 baada ya kustaafu.
“Kwa msimu huu wa tano tumekuwa na utaratibu wa kutoa fedha kwa viongozi waliostaafu ikiwa ni sehemu ya malipo kwa kazi walioifanya ya kuongoza kijiji kwa wiki mbili,” alisema Babu Rajabu.
Aliwataja viongozi hao wastaafu kuwa ni Irene Ishengoma, Aloyce Sambuta na Olive Kiarie.