33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Makatibu wakuu watembelea mpaka

Mwandishi Wetu-Dar es salaam

MAKATIBU wakuu kutoka Ofisi ya Rais- Tamisemi, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wamefanya ziara wilayani Ngara, Mkoa wa Kagera kukagau  uimarishaji wa mpaka uliofanyika mwaka 2014.

Ziara hiyofanyika mwishoni mwa wiki, iliyojumuisha wataalamu mbalimbali wanaoshughulikia mpaka wa kimataifa kati ya Tanzania na nchi zinazoizunguka, ambapo wajumbe walitembelea baadhi ya maeneo yaliyopitiwa na uimarishaji mpaka lililofanyika mwaka 2014.

Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Florence Turuka ambaye ni mwenyekiti wa wajumbe hao alisema, lengo la kutembelea na kukagua maeneo ya mpaka wa kimataifa uliopitiwa uwekaji wa alama za hifadhi ya mpaka (vigingi) mwaka 2014, ni kukusanya taarifa kutoka kwa wananchi.

Alisema taarifa itakayotolewa na wananchi maeneo yaliyopitiwa na uimarishaji wa mpaka, itaisaidia Serikali kujua, ni mikakati gani iwekwe  maeneo yanayozunguka mpaka ili kuwalinda wananchi pamoja na mali zao.

Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Luteni Kanali Michael Mtenjele, alisema mpaka kati ya Tanzania na Burundi uko salama na wilaya imeendelea kuwa na uhusiano na mawasiliano ya karibu na nchi hiyo.

Alisema mara nyingi zinapotokea changamoto mawasiliano ya simu hufanyika na nchi ya Burundi na kuyatatua kitu ambacho kisingewezekana kama mahusiano yangekuwa siyo mazuri.

“Taarifa ya wilaya pia ilibainisha uimarishaji mpaka lililofanyika mwaka 2014, liliwaathiri baadhi ya wananchi wa Tanzania waliokuwa wanaishi mpakani,” alisema Kanali Michael.

Pamoja na athari ambazo wilaya ilishabainisha, wajumbe wanaweza kupata taarifa zaidi kuhusu hali ya mpaka kutoka kwa wananchi wanaoishi mpakani watakapokuwa wanatembelea na kukagua maeneo hayo.

Jesca Lameck mwenye umri kati ya miaka 75-80, ni mmoja kati ya wananchi waliosema uimarishaji wa mpaka la mwaka 2014 lilimuathiri.

Alisema alijikuta sehemu ya shamba lake la miti, kahawa, matunda na makaburi vikiangukia upande wa nchi ya Burundi.

Baada ya kutembelea na kufanya mikutano na wananchi waliopitiwa na Florence Turuka, alipokea taarifa kuhusu athari zilizotokana na na changamoto nyingine zinazohusu mpaka tofauti na za uwekaji alama za hifadhi ya mpaka.

Aliushukuru uongozi wa wilaya unavyosimamia uhusiano na nchi ya Burundi na kuahidi kuifikisha mbele zaidi taarifa aliyoipata kuhusu changamoto za mpaka wa Tanzania na Burundi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles