27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Wafanyakazi watakiwa kutambua haki zao

Brighiter Masaki -Dar es salaam

KAIMU Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Said Rwamba amewataka wafanyakazi kutambua haki na wajubu wao wanapokuwa maeneo ya kazi ili  kupata haki za msingi kwa wakati.

Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, wakati wa  uzinduzi wa kampeni maalumu iliyoshirikisha wadau kutoka serikalini na sekta binafsi walipokuwa wakijadili changamoto wanazokumbana nazo wafanyakazi maeneo ya kazi.

Alisema katika kampeni hiyo, kikubwa wanaangalia zaidi ni namna ya kusaidia wafanyakazi waliopo katika ajira ambazo hazileti maendeleo kwa wafanyakazi.

“Tunahitaji elimu iongezeke kwa wafanyakazi waliopo mijini na vijijini ili waweze kutambua haki zao tukishirikiana na Serikali, tunaamini wafanyakazi wakipata elimu ya kutosha, kujitambua hata kesi dhidi ya manyanyaso kutoka kwa waajiri wao zaitapungua,” alisema.

Alisema ni wajibu wa kila mfanyakazi kuwa na mkataba kulingana na elimu yake.

Alisema sheria inamtaka kila mwajiri kumlipa mfanyakazi mshahara atakaohakikisha unakidhi mahitaji yake.

 “Tutambue wafanyakazi ni binadamu,waajiri wanatakiwa waboreshe maeneo ya kazi, kuwa salama na rafiki kwa mfanyakazi, huku akihakikisha mfanyakazi anapokea malipo yake kwa wakati ulio sahihi,”alisema.

Wakili na Mtafiti wa Sheria na Haki za Binadamu kutoka katika kituo cha LHRC, Joyce Komanya alisema zipo changamoto nyingi wanazokutana nazo kutatua matatizo ya wafanyakazi,kubwa zaidi ni suala la haki na sheria za wafanyakazi kutokufuatwa.

Alisema wanahitaji ushirikiano wa kutosha kutoka katika vyama vya wafanyakazi pamoja na wafanyakazi wenyewe kupiga kelele wanapoona wanatendewa vitendo visivyo stahili.

“Tunachojaribu kufanya ni kuibua yale matatizo yaliyopo ndani kabisa kwa wafanyakazi, zipo changamoto za aina mbili za kiafya pamoja na kiakili,unakuta mfanyakazi anaumia anapikuwa eneo la kazi na pia kudumaa kwa akili awapo kazini lakini kampuni haihusiki kwa chochote.

“Wafanyakazi ni wajibu wao pia kudai haki zao wanapoona mambo yanaenda tofauti na sheria inavyosema sisi tutaendelea kuwapigania wafanyakazi tukishirikiana na wadau pamoja na serikali pia,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles