33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Majangili wanaswa na bunduki 21

Photo-1Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MSAKO mkali dhidi ya watu wanaodaiwa kuwa majangili umeanza kuzaa matunda  baada ya watu wanane kutiwa mbaroni wakiwa na bunduki 21 zikiwamo   ambazo zinadaiwa kuwa za vita.

Habari za uhakika ambazo MTANZANIA ilizipata jana na kudhibitishwa na Waziri wa Malisili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, zinasema watu hao walikamatwa katika Hifadhi ya Taifa ya Selous wakiwa kwenye harakati za ujangili.

Tumekamata watu wanane wakiwa na silaha nzito nzito katika Hifadhi ya Selous mkoani Morogoro, naamini hawa ni miongoni mwa magenge ya uhalifu ambayo yamekuwa yakitukosesha usingizi.

“Msako wetu umeanza kuzaa matunda, nasema huu ni mwanzo tu, kazi bado ni kubwa na hatukati tamaa hata kidogo.

“Tunataka kuona rasilimali zetu hazichezewi na watu wasiolitakia mema Taifa hili,”alisema Profesa Maghembe.

Alisema tayari watuhumiwa wote wamekabidhiwa kwa jeshi la polisi mkoani humo  hatua za sheria zichukuliwe baada ya upelelezi kukamilika.

Kamanda wa Polisi Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paul alipotafutwa na gazeti hizi kuzungumzia suala hilo, hakukubali wala kukataa, huku asisitiza kuwa ametingwa na vikao vingi.

Licha ya kupokea simu yake ya kiganjani mara mbili, Kamanda Paul aliendelea kushikilia msimamo wake wa kutotoa ufafanuzi wa tukio hilo.

“Mwandishi nina kikao kirefu, nakuomba unitafute baadaye juu ya suala hilo…husikii nachokwambia jamani?”alisema Kamanda Paul.

Baada ya kupita karibu saa mbili, gazeti hili lilimtafuta tena, lakini simu yake ikapokelewa na mtu aliyejitambulisha kuwa mlinzi wake.

“Mimi ni mlinzi wa afande Paul, yuko kikaoni unasemaje ndugu yangu…nakushauri uandike ujumbe mfupi wa maneno (sms), nitampelekea kikaoni,”alisema msaidizi huyo.

Pamoja na kutumiwa ujumbe huo hadi tunakwenda mitamboni haukujibiwa.

Akizungumzia msako mkali unaondelea katika pori la akiba la Maswa wilayani Meatu mkoani Simiyu, Waziri Maghembe alisema leo anatarajia kukutana na waandishi wa habari kuelezea mafanikio yaliyofikiwa katika tukio hilo.

Wiki iliyopita katika pori hilo, majangili yaliitungua kwa risasi helkopita na kumuua rubani wake, Kapteni Gower Roger.

“Nakuomba uwe mvumilivu kesho (leo), nitakutana na waandishi wa habari kupasua jibu kuhusu tukio la Maswa.  Tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa…kuwa na subiri ndugu yangu,”alisema Waziri Maghembe.

Kapteni Roger  alikuwa anashirikiana  na askari wa wanyamapori ambao wamekuwa wakipambana na majangili kwenye pori hilo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles