|Anna Potinus, Dar es Salaam
Rais John Magufuli, amewataka viongozi wa Jiji la Dar es salaam, wametakiwa kujitafakari katika utendaji kazi wao kwani imeonekana kukwama katika sekta mbalimbali ikilinganishwa na majiji mengine.
Kauli hiyo ameitoa leo katika hafla ya uapishwaji wa viongozi walioteuliwa wakiwamo Wakatibu wa Wakuu wa wizara mbalimbali, Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala iliyofanyika Ikulu jijini.
Rais Magufuli amesema kumekuwa na ‘upigaji’ mkubwa huku viongozi wakiangalia bila kuchukua hatua zozote.
“Juzi nilikuwa naongea na mabalozi, nikawaambia Dodoma ndiyo inaongoza katika majiji, manispaa, wilaya Tanzania nzima hivyo unaweza ukajiuliza kuna nini unaweza ukajua hapa Dar es salaam kuna upigaji na viongozi wapo,” amesema Magufuli.
Amesema viongozi wa Dar es salaam wakikutana kwenye vikao wanakaa siku mbili lakini zitajazwa ni siku nne hivyo kwa namna hiyo hawawezi kupata mapato kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.
“Utakuta hata wamachinga wanasimama barabarani hawana mahali pa kufanyia biashara, wakina mama wamedhulumiwa lakini viongozi wapo hivyo nataka niwaambie viongozi mlioteuliwa hakuna mwenye garantii ya kazi,” amesema Rais Magufuli.
Mh.Rais wetu mpendwa JPM tunakuombea kwa Mungu Kula itwapo Leo, katika uteuzi Wako upate viongozi wenye Nia njema kama wewe kwa maendeleo ya Taifa letu. Usitusahau vijana tulioshiriki kwenye kampeni za 2015 tukitokea shirikisho la vyuo vikuu.