26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

STIGGLER’S GORGE KUENDESHA TRENI YA UMEME

|Bakari Kimwanga, Morogoro



Waziri wa Nishati,  Dk. Medard Kalemani, amesema umeme wa mradi wa umeme wa Stiegler’s Gorge ndiyo utatumika kuendeshea treni mpya ya umeme.

Dk. Kalemani ameyasema hayo leo Mjini Morogoro, kwenye kikao cha mawaziri na makatibu wakuu ambao wizara zao zinatekeleza mradi huo.

“Mradi huu  utazalisha Megawati 2,100 na ndiyo utakaotumika kuendeshea treni ya kisasa ya umeme ya  Standard Gauge.

“Hivyo tumekutana hapa kujadili taarifa ya wataalamu kuhusu mradi, kutafakari changamoto na kuzifanyia kazi pamoja na kutembelea eneo la mradi,” amesema Dk. Kalemani.

Pia Waziri huyo wa Nishati, amesema Serikali itachukua hatua za kisheria kwa yeyote atakayekwamisha uwekezaji wa mradi huo ambao unahusisha wizara 11.

Kikao hicho kimewakutanisha watalaamu na viongozi wengine mbalimbali wakiwamo  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles