27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli kupita wilaya moja hadi nyingine Mtwara

Na FLORENCE SANAWA

– MTWARA

MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Bayakanwa, amesema Aprili 2 mwaka huu mkoa unatarajia kupokea ugeni wa Rais John Magufuli, ambaye atafanya ziara ya siku mbili na kutembelea miradi mikubwa sita.

Kati ya miradi hiyo sita, mitano ataweka jiwe la msingi na mmoja atauzindua rasmi.

Mwaka 2017 Rais Magufuli alitembelea mkoa huo na kuahidi kurudi tena  kuweka jiwe la msingi katika Barabara ya Uchumi inayotoka Mtwara kuelekea Tandahimba na Newala, ambayo imeshaanza kutengenezwa kwa kiwango cha lami kwa kilomita 50 kutoka Mtwara hadi Mnivata.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu huyo wa Mkoa alisema katika ziara hiyo, Rais Magufuli ataweka jiwe la msingi upanuzi wa uwanja wa ndege, Barabara ya Uchumi Mtwara – Mnivata kilomita 50, Kiwanda cha Yalin cha kubangua korosho cha mtu binafsi, Chuo cha Ualimu Kitangali, Kituo cha Afya Kwa Mbonde Masasi na kuzindua Barabara ya Mangaka Mtambaswala na Mangaka Nakapanya.

Alisema kutokana na ukubwa wa miradi na umuhimu wa ugeni huo mkubwa, wananchi wanatakiwa wajitokeze kwa wingi katika maeneo hayo.

“Natumia nafasi hii kuwaalika wakazi wote wa Mkoa wa Mtwara katika ziara ya kikazi ya Rais, ambapo atakuwepo kwa muda wa siku mbili katika mkoa huu ili kushuhudia akiweka jiwe la msingi na kuzindua miradi hii mikubwa ambayo tunaamini itachochea kukua kwa uchumi Mkoa wa Mtwara,” alisema.

“Kwetu sisi tunaona kama tumepata upendeleo, kwa kuwa ni mara ya pili Rais kuja katika mkoa wetu na safari hii atapita katika wilaya zote ndani ya Mkoa wa Mtwara, wananchi wajitokeze ili wapate fursa ya kukutana na Rais wao katika kipindi hiki cha ziara ya siku mbili,” alisema Byakanwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles