31.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli awatolea uvivu wapelelezi

Anna Potinus

Rais John Magufuli amewatolea uvivu wapelelezi wa kesi nchini kwa kutofanya kazi zao ipasavyo na badala yake wamekuwa wakiwaumiza wengi kwa kuwaweka magerezani watu wasiokuwa na hatia.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Febuari 2, walipokuwa akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Sheria yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.

“Bado kuna changamoto kubwa kwa upande wa wapelelezi hivyo ninawaomba wapelelezi na wasimamizi wa sheria mfanyie kazi hili kwani watu wanateseka mimi nimeshuhudia ukienda kwenye magereza yetu watu wanalia na wengine ni kesi za kusingiziwa wapo wengine wamewekwa kule ndani kwasababu ya matajiri kwamba ni akukomesha utaenda kwanza mahabusu.

“Wapelelezi ninyi ufalme wa mbinguni utakuwa shida kwenu msipotubu na kumrudia Mungu kwasababu roho za watu wasiokuwa na hatia zinaangamia kule gerezani na wala msiwasingizie majaji na mahakimu kwasababu hamuwapelekei na saa nyingine hata kupelekwa mahakani ni lazima uhonge ili kesi yako isomwe, mnawapa shida mahakimu na majaji ninawaambia ukweli mtakwenda kuyalipa badilikeni,” amesema Rais Mgufuli.

Aidha ameongeza kuwa kwa sasa wanafanya majadiliano ya kuwarejesha mwakwao raia wa kigeni wakiwamo Waethiopia 1415 ambao wamefungwa kwenye mahakama za Tanzania kutokana na matatizo ya uhamiaji.

“Tunafanya mazungumzo na ninafikiri nitasaini hati mapema ndani ya siku mbili tatu ili hawa wafungwa waweze kurudiswha kwao na hii pia itatusaidia kupunguza wafungwa wanaokaa mahakamani,” amesema Rais Magufuli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles