27 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

MADURO ASHINDA UCHAGUZI, WAPINZANI WATAKA URUDIWE

CARACAS, VENEZUELA


TUME ya Uchaguzi ya Venezuela, imemtangaza Rais Nicolas Maduro kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika juzi, ambao upinzani unataka urudiwe.

Akiwahutubia maelfu ya wafuasi wake nje ya Ikulu yake mjini Caracas kufuatia ushindi huo, Rais Maduro ameusifia akiutaja kuwa wa ‘kihistoria’.

“Haijawahi kutokea kwa mgombea wa urais kupata asilimia 68 ya wingi wa kura.

“Tumeshinda tena! Ushindi wa kishindo! Sisi ni kani ya historia iliyogeuka kuwa ushindi mkubwa,” alisema Maduro huku akishangiliwa na wafuasi wake.

Hata hivyo, upinzani umeupinga uchaguzi huo ukisema si halali na wametaka uchaguzi mpya uandaliwe baadaye mwaka huu.

Mpinzani mkuu wa Maduro, Henri Falcon aliyetangazwa kupata asilimia 21.2 ya kura dhidi ya 67.7 alizopata Maduro, amewaambia wanahabari kuwa mchakato mzima wa uchaguzi ulikuwa batili.

“Kwetu, hakuna uchaguzi uliofanyika. Tunapaswa kufanya uchaguzi mpya unaoeleweka Venezuela,” alisema.

Katika taifa hilo linalokumbwa na mzozo mbaya wa kiuchumi, asilimia 46 ya wapigakura pekee ndio waliojitokeza.

Aidha jumuiya ya kimataifa pia imeukosoa uchaguzi huo, ambao sasa unampa Maduro nafasi ya kutawala kwa muhula wa pili hadi mwaka 2025.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles