BEYONCE ANUNUA KANISA MAREKANI

0
851

NEW YORK, MAREKANI


MWANAMUZIKI wa Marekani, Beyonce Knowles, amekuwa mmiliki mpya wa Kanisa la New Orleans Church, ambalo lina umri wa zaidi ya miaka 100.

Beyonce alinunua kanisa hilo ambalo lilikuwa likinadiwa kwa Dola za Kimarekani 850,000 sawa na Sh 1,938,000,000.

Kanisa hilo ambalo lilijengwa mwaka 1900’s,  lilikuwa halitumiki kwa ibada kutokana na kukosekana kwa viongozi wake, ambao baadhi yao wanadaiwa kufariki hivyo hatua  ya mwanamuziki huyo ni dhamira ya kutaka kuliendeleza.

Zoezi la ununuaji wa kanisa hilo, ulifanya Kanisa la San Francisco  anapofanyia ibada Beyonce kwa mara ya kwanza, kujaza watu zaidi ya 900.

Kanisa la New Orleans Church lipo karibu na anapoishi mdogo wake, Beyonce, ambaye ni Solange hivyo itakuwa rahisi kwake kupata watu walio tayari kujiunga na kupata mafunzo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here