31.3 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

Madaktari bingwa Temeke kuweka kambi Buza

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Madaktari bingwa wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke wanatarajiwa kuweka kambi ya siku tano katika Kituo cha Afya Buza ili kutoa huduma za uchunguzi wa magonjwa mbalimbali.

Madaktari hao watatoa huduma hiyo kuanzia Januari 22 hadi 26 mwaka huu lengo likiwa ni kuwawezesha wananchi kupata huduma za kibingwa karibu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Januari 18,2024 na Ofisa Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma wa Hospitali ya Temeke, Cleopatra Mokiwa, kambi hiyo itahusisha utoaji huduma za matibabu ya kiuchunguzi wa kibingwa na bingwa bobezi katika kituo hicho.

Amesema kambi hiyo itahusisha matibabu ya kibingwa ya magonjwa ya ndani, macho, pua, masikio na koo, kinywa na meno, wanawake na uzazi, upasuaji, mifupa, afya ya akili, upasuaji wa njia ya mkojo, utengamao, huduma za watoto pamoja na uchangiaji damu wa hiyari.

Ofisa huyo amesema uwepo wa kambi hiyo ni mojawapo ya mikakati ya hospitali hiyo katika kuhakikisha huduma za kibingwa zinawafikia moja kwa moja wananchi.

“Tunatambua umuhimu wa afya bora katika kuboresha maisha ya jamii yetu, hivyo tunaleta huduma za kibingwa karibu na wakazi wa eneo letu. Tunawakaribisha wote wanaoishi ndani na nje ya Temeke kujitokeza kwa wingi na kuchangamkia fursa hii ya kupata huduma bora za kibingwa,” amesema Mokiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles