25.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 15, 2024

Contact us: [email protected]

Mabasi ya Kilimanjaro yatolewa kifungoni

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA),imeruhusu Kampuni ya mabasi ya Kilimanjaro kuendelea kutumia rasmi leseni na ratiba za mabasi yake 35 baada ya kutekeleza masharti iliyopewa.

Januari 6, 2024 kampuni hiyo ilisitishiwa leseni na LATRA baada ya kukiuka masharti kwa kutoa huduma bila kutumia mfumo wa tiketi mtandao na kutoza nauli zaidi ya viwango vilivyoidhinishwa na mamlaka husika.

Akitoa taarifa hiyo leo Januari 14, 2024 jijini Dar es Salaam kwa waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Habibu Suluo amesema mabasi hayo yataanza kufanya kazi kuanzia leo baada ya kukamilisha masharti iliyopewa.

Amesema kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kikosi Cha Usalama Barabarani pamoja na kituo Cha Taifa Cha kuhifadhi kumbukumbu (NIDC) imehakiki mfumo wa tiketi mtandao wa kampuni hiyo.

“Kabla ya kuruhusiwa kampuni hiyo ilitakiwa kutekeleza masharti iliyopewa ikiwemo kutumia mfumo wa tiketi mtandao, kuzingatia viwango vya ukomo wa nauli zilivyowekwa na LATRA,” amesema Suluo.

Mbali na mfumo huo pia ilipaswa kuwasilisha maombi ya kurejesha huduma ambayo itaiwezesha LATRA kuhakiki mfumo wa tiketi mtandao, nauli zilizoigizwa kwenye mfumo na madaraja ya mabasi hayo 35 kabla ya kuruhusu leseni na ratiba za mabasi husika kuendelea kutumika.

“LATRA inapenda kutoa taarifa kuwa imeruhusu leseni na ratiba za mabasi 35 ya Kilimanjaro Truck Company Limited kuanza kutumika kuanzia leo Januari 14 hii ni baada ya kutimiza masharti ,”amesema.

Aidha amewataka watoa huduma wote kufanya kazi kwa mujibu wa sheria ili kuepuka kuchukukuliwa hatua mbalimbali.

Naye Mwanasheria wa kampuni hiyo, Dickson Ngowi aliishukuru LATRA kwa ushirikiano iliotoa pindi ilivyositishiwa leseni na kuhaidi masharti yote waliyopewa wataendelea kuyatekeleza.

“Magari yetu yote yamekaguliwa na yamepewa stia maalumu ambapo mlangoni kabisa yamebandikwa daraja husika la gari ili kumsaidia abiraia kujua anapanda gari la daraja gani,”amesema Ngowi

Kwa upande wake Mratibu mwandamizi wa Polisi Salumu Morimori aliwaomba watoa huduma kuzingatia sheria za mamlaka husika ikiwemo kutii sheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles