30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Lugola awaonya wachochezi wanaojipenyeza kwa kivuli cha dini

Felix Mwagara, Bunda

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewaonya baadhi ya watu wanaojipenyeza kupitia mgongo wa taasisi za dini nchini kwa kujifanya wahubiri kumbe niwachochezi na wanaingiza masuala ya kisiasa.

Aidha, amesema wizara yake ipo makini katika mchakato wa kusajili makanisa na misikiti yote nchini na hadi sasa kuna maombi mengi ambayo yametumwa wakiomba kusajiliwa.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Sunsi, Jimbo la Mwibara, mkoani Mara, Lugola ambaye ni mbunge wa jimbo hilo, amesema taasisi za dini zina mchango mkubwa nchini na uwepo wao ni muhimu katika maendeleo ya nchi na serikali inathamini mchango wao katika kuimarisha amani na pia kuwaweka watu pamoja.

Amesema kuna baadhi ya dini hizo zinakiuka utaratibu wa usajili na kuvunja sheria zanchi kwa kuacha kuhubiri masuala ya kiroho wanajihusisha na masuala ya kisiasa nauchochezi.

“Aidha, kuna baadhi ya makanisa bado hayajasajiliwa kwa sababu tunahitaji umakini mkubwa katika kufanya uchunguzi wa kina kabla hatujatoa usajili kwa lengo la kuepusha baadhi ya taasisi za dini zenye mpango mbaya na maendeleo ya nchi. 

“Serikali hii haitakuwa tayari kwa mwananchi yeyote kutumia mwamvuli wa dini au kufanya misikiti na makanisa kuwa kichaka kwa kufanya uchochezi nchini na kuhatarisha amani ya nchi tuko makini na hatuwezi kuchezewa na mtu yeyote au taasisiyoyote,” amesema Lugola.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles