26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Mel B avunjika mbavu


LONDON, ENGLAND

STAA wa muziki na filamu nchini Uingereza, Melanie Brown, maarufu kwa jina la Mel B, amethibitisha kuvunjika mbavu mbili na kuumia mkono baada ya kuanguka nyumbani kwa rafiki yake jijini London.

Kwa mujibu wa mtandao wa US TV, msanii huyo amekuwa akikaa kwa rafiki yake kwa kipindi chawiki moja sasa, hivyo juzi alijikuta akianguka wakati anatoka nje ya nyumba hiyo na kusababisha kuumia mkono na kuvunjika mbavu mbili.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 43, bado yupo hospitalini kwa ajili ya matibabu, lakini hali yakeinadaiwa kuendelea vizuri.

Baadhi ya mashabiki wamekuwa wakitumia mitandao yao ya kijamii na kudai sababu za msanii huyo kuanguka ni kutumia dawa za kulevya kupita kiasi. Hadi sasa hakuna taarifa rasmi ya kuanguka kwake.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,277FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles