27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

KOREA KASKAZINI ILINUNUA TEKNOLOJIA UJERUMANI

BERLIN, UJERUMANI


KITUO cha Utangazaji cha Umma nchini Ujerumani (NDR) kimeripoti kuwa Korea Kaskazini iliutumia ubalozi wake mjini Berlin kujipatia vifaa vya teknolojia ya juu.

Kwa mujibu wa Shirika la Upelelezi wa Ndani (BfV), teknolojia hiyo ilitumika katika programu ya makombora na mpango wa nyukilia wa Korea Kaskazini.

Mkurugenzi Mkuu wa BfV, Hans-Georg Maassen alikaririwa akieleza hayo wakati akihojiwa na  kituo cha NDR Jumatatu wiki hii.

Alisema Korea Kaskazini ilinunua vifaa na teknolojia kwa ajili ya programu ya makombora ya masafa marefu kwa kutumia ubalozi wake mjini Berlin.

“Tuligundua hilo lilitokea pale, kulingana na mtazamo wetu katika programu ya makombora pamoja na mpango wa nyukilia,” alisema Hans-Georg Maassen.

Ingawa hakusema wazi ni aina gani ya teknolojia na vifaa vilivyonunuliwa, Maassen amesema vilikuwa ni vifaa vyenye matumizi ya aina mbili; kiraia na ya kijeshi.

“Tunapogundua kitu kama hicho, tunakizuia. Hatuwezi kutoa uhakika kuwa tunaweza kugundua kila kitu na kuzuia visa vyote,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles