Grace Shitundu
Suala la kuwa ardhi katika baadhi ya maeneo imechoka hata kusababisha kusiwa na mazao bora imekuwa likisemwa na baadhi ya wakulima na wataalamu wa kilimo.
Hali ambayo imekuwa ikiwafanya baadhi ya wakulima kutumia mbolea nyingi zenye kemikali ili kuweza kupata mazao yenye ubora na wingi kama zamani.
Suluhisho la changamoto hiyo inaelezwa kuwa ni kufanya kilimo mchanganyiko ‘crop rotation’ .
Aina hii ya kilimo huzingatiwa kwa kulimwa mazao tofauti katika shamba moja katika muda ambao umepangiliwa.
Kupanda mazao kwa mzunguko ina maana ya kuwa na aina mbalimbali ya mazao katika eneo moja kwa msimu.
Kwa mfano, kama shamba limepandwa mahindi na maharage kwa kipindi cha mwaka mmoja, mkulima anaweza kubadili mzunguko kwa kupanda aina nyingine ya mazao katika eneo hilo kwa mwaka(msimu) unaofuata.
Mimea iliyo inayoshauriwa zaidi katika kilimo cha mzunguko ni pamoja na jamii ya kunde, au malisho kama leusina ambayo husaidia kuongeza rutuba kwenye udongo.
Endapo mkulima zao moja katika shamba lile zaidi ya misimu miwili wadudu na magonjwa,huwa sugu katika shamba hilo hivyo basi katika kilimo cha mzunguko
Mazao tofauti huchukua virutubisho tofauti katika ardhi na kuiacha ardhi kutokuwa na uwiano sawa wa rutuba..
Kuna mazao ya aina tofauti ambayo yanaweza kupandwa shambani katika kilimo mzunguko ambayo ni kama viazi vitamu, mihogo, karoti (mazao ya mizizi), mahindi, mtama (mazao ya nafaka), ufuta, alizeti (mazao ya mafuta), maharage, mbaazi, kunde (mazao jamii ya mikunde), katani, pamba (mazao ya nyuzi), nyanya, kitunguu, kabichi, ngogwe (mazao ya mboga mboga ), tikiti maji, zabibu, nyanya (mazao yenye mizizi mirefu), maharage, kabichibichi, matango, biringanya, spinachi, kitunguu (yenye mizizi mifupi)
Kanuni za kilimo cha mzunguko.
Mazao ambayo huchukua rutuba nyingi katika udongo mazao hayo huitwa ‘heavy feeder’, na mazao mengine huchukua rutuba kidogo katika udongo huitwa ‘light feeders’, katika kupangilia ubadilishaji wa mazao heavy feeder yabadilishane na light feeders au kinyume chake.
Mazao ambayo yana mizizi mifupi yabadilishane na mazao yenye mizizi mirefu,kwasababu mazao yenye mizizi mirefu huchukua kiasi kingi cha unyenyevu uliopo katika ardhi.
Mazao ambayo hutoka katika familia moja hushambuliwa na wadudu na magonjwa yanayofanana, hivyo ni vyema mazao yabadilishwe kutokana katika familia tofauti.
Mfano shamba lilopandwa zao jamii ya ‘solanaceae’ kama nyanya libadilishwe na zao lililo katika familia tofauti.
Mazao tofauti yana tabia tofauti katika ukuaji wake,kwa mfano viazi vitamu hutambaa na kufunika udongo na kupelekea magugu kutopata nafasi ya kukua,hivyo katika kilimo cha mzunguko mazao anayotambaa yahusike.
Pia katika kilimo cha mzunguko inashauriwa kupanda mazao jamii ya mikunde,mazao haya husaidia sana kuongeza rutuba ya udongo kwani hujitengenezea rutuba yenyewe, mfano wa mazao haya ni maharage,mbaazi,na kunde.
Faida za kilimo cha mzunguko.
Wataalamu mbalimbali wa kilimo wanatoa faida za kulima kwa mzunguko kuwa ni pamoja na husaidia kuweka uwiano wa rutuba ardhini kwani kuna mazao ambayo huhitaji nyingi na mengine huhitaji rutuba kidogo.
Hivyo rutuba ya udongo hutumika vyema na mazao yatakayo badilishana, na hasa mazao ya jamii ya mikunde yanapopandwa kwani husaidia kuongeza rutuba ya udongo.
Wataalamu wanaeleza kwamba kilimo mzunguko pia husaidia katika kudhibiti wadudu na magonjwa.
Inaelezwa kwamba zao la aina mmoja linapopandwa mfululizo katika misimu tofauti huchangia kuenea kwa magonjwa na na huwa kuna gharama nyingi za kuzuia magonjwa kwa kutumai viuatilifu hivyo kuzungusha mazao hupunguza au kuondoa kabisa magonjwa hayo.
Pia ni udhibiti wa wadudu kwani wadudu kama minyoo fumba huwa na tabia ya kung’ng’ania shambani hivyo endapo mkulima atarudia aina ile ile ya zao udhibiti waki huwa ni mgumu.
Mambo muhimu
Mambo muhimu ambayo mkulima anatakiwa kuzingatia ni kuhakikisha anabadilisha mazao kulingana na aina ya mazao na uhitaji wake wa rutuba.
Ni vizuri mkulima akaweka mpango mzuri wa kuachanisha mazao katika shamba lake, kwa kuandaa kalenda nzuri ya uzalishaji.
Mfano msimu wa kwanza yakipandwa mahindi unafuata iwe ni maharagwe kisha ifuate mihogo