26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

Kesi ya baba kumlawiti, kumbaka binti wake wa miaka 10 kuanza kunguruma Njombe

Elizabeth Kilindi – Njombe               

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Njombe leo inatarajiwa kuanza kusikiliza ushahidi wa Jamhuri katika kesi ya inayomkabili Ezroni Ndone(44) Mkazi wa Joshoni mjini Njombe, anayedaiwa kumbaka na kumlawiti mtoto wake.

Shauri hilo namba 14 la mwaka 2020 linasikilizwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Njombe, Hassan Makube.

Awali mawakili wa Serikali Nuru Minja na Andrew Nandwa, waliiomba mahakama kufanya mabadiliko chini ya kifungu kidogo cha kwanza cha sheria ya mwenendo ya makosa ya jinai sura ya 20 marejeo 2002 kubadilisha hati ya mashitaka umri wa muathirika wa tukio usomeke miaka 10 badala ya 11 kama inavyosemeka kwenye kosa la kwanza na pili.

Shauri liliendelea kwa kusomwa hoja za awali ambapo wakati upande wa Jamhuri ukiwakilishwa na wakili wa serikali Minja na Mandwa upande wa mshtakiwa unawakilishwa na wakili Emmanuel Chengula.

Mara baada ya kusikiliza hoja za awali, Hakimu Makube alihairisha kesi hiyo hadi Februari saba kwa ajili ya hatua kusikiliza ushahidi wa Jamhuri.

Hata hivyo mstakiwa huyo ameshindwa kutimiza masharti ya dhamana kwa sababu alitakiwa awe na bondi ya Sh milioni 10 na wadhamini watatu wawili kati yao wawe wanatoka taasisi zinazotambulika na wathibitishe.

Kesi hiyo imeonekana kubeba hisia kwa wananchi wa Njombe hali iliyopelekea kujaa kwenye chumba cha mahakama na wengine kuzuiwa kuingia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles