25.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Asilimia 50 ya simba duniani wapo Tanzania

Mwandishi wetu – Serengeti

TANZANIA ni kitovu cha simba duniania baada ya kuwa na simba kati ya silimia 40- 50 za simba duniani  katika hifadhi za Taifa.

Akizungumza jana kabla ya kuanza kwa zoezi la kuwahamisha simba 17 kutoka ikolojia ya Serengeti mkoani Mara kwenda hifadhi ya Taifa ya Burigi – Chato mkoani Geita, mtafiti wa simba kutoka Taasisi ya Utafiti wa wanyamapori nchini (Tawiri), Dk. Dennis Ikunda alisema hali hiyo inatokana na jitihada zinazozofanywa katika kuboresha uhifadhi endelevu nchini.

Alisema pia hao asilimia 50 ya simba wa Tanzania wanapatikana katika ikolojia ya Serengeti na hivyo kusema mamlaka husika katika hifadhi hiyo imekuwa ikijitajidi kuhakikisha kunakuwepo na uhifadhi endelevu  katika eneo hilo.

Alisema kutokana na uhifadhi huo endelevu, wamegundua idadi ya simba imeongezeka katika ikolojia ya Serengeti na hivyo kuwa kubwa zaidi ya uwezo wake hali ambayo imekuwa ikisababisha simba kutoroka na kuingia katika makazi ya watu kufanya uharibifu.

Alisema kutokana na ongzeko hilo mamlaka husika zimeamua kuwahamishia baadhi ya simba katika hifadhi ya Taifa ya Burigi ambako kuna idadi ndogo ya wanyama hao.

Dk. Ikunda alisema kabla ya kuhamishiwa huko, simba hao walifungiwa katika boma maalum kwa zaidi ya siku 20 lengo likiwa ni kuwafanya wazoee mazingira mapya ambayo wataenda kuishi.

“Kwavile kule Burigi kwa mujibu wa utafiti chakula kikuu ni pundamilia, baada ya kuwakamata tumekuwa tukiwapa nyama ya pundamilia ili wakifika kule wasipate shida, wawe wamezoea kwahiyo hatuna wasiwasi tayari wameshazoea hali hiyo” alisema mtafiti huyo.

Naye Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (Senapa), Misana Mwishawa, alisema lengo la simba hao kuhamishiwa katika hifadhi ya Burigi ni kutaka kuboresha na kuimarisha utalii katika hifadhi hiyo na nchini kwa ujumla.

Alisema simba ni miongini mwa vivituo vikuu vya utalii nchini hivyo maamuzi ya kuwahamishia katika hifadhi hiyo ambayo ina simba wachache yalilenga katika kuboresha sekta ya utalii huku akifafanua kuwa suala la kuhamisha wanyama kutika katika hifadhi moja kwenda nyingine ni la kawaida na hufanyika kutokana na uhitaji.

Alisema kuwa kabla ya kuwahamisha lazima utafiti wa kitaalam unafanyika ili kujiridhisha na kwamba kutokana na simba kuwa wengi maamuzi hayo yanalenga kuhakikisha kuwa idadi ya simba inaendena na ukubwa wa mazingira katika ikolojia ya Serengeti.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, alisema sekta ya utalii ina mchango mkubwa katika uchumi wa nchi hivyo ni vema ikafanywa kuwa endelevu na kusema kuwa zoezi la kuwahamisha simba kutoka Serengeti kwenda Burigi ni moja ya mkakati wa kuendeleza sekta hiyo.


- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,530FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles