31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

Kenya: William Ruto atishia kukihama chama tawala

Nairobi, Kenya

Naibu Rais wa Kenya William Ruto ametishia kukihama chama cha Jubilee iwapo kitaendelea kuwavuruga viongozi wanaogemea upande wake, huku akisema yuko tayari kukitumia chama kipya UDA kugombea kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Katika mahojiano na kituo kimoja cha televisheni nchini Kenya, Ruto aliyeonekana kuzidiwa na jazba, alisikitishwa na jinsi wabunge wanaoegemea upande wake walivyotimuliwa kwenye nafasi za uwenyeviti wa kamati za bunge na baadhi ya mawaziri pia kuondolewa na kushtakiwa kwa kuhusika kwenye ufisadi.

Seneta wa Elgeyo-Marakwet, Kipchumba Murkomen, aliondolewa kwenye wadhfa wa kiongozi wa wengi katika bunge la seneti huku mwenzake wa Nakuru Susan Kihika, akiondolewa kuwa kiranja. Hata hivyo Ruto amesisitiza kuwa bado anamheshimu rais Uhuru Kenyatta.

“Ningali na matumaini kwamba chama cha Jubilee kitabadilika na kurejea kwenye maono ya kwanza, lakini hilo lisipofanyika, lazima tuwe na mikakati, sisi tuna bahati kwa sababu tuna chama cha UDA. Jubilee ikiendelea kutuvuruga, lazima ufikirie,” alisema William Ruto.

Mapema mwaka huu, Chama cha Jubilee kilipendekeza kutimuliwa kwa maseneta maalum wanaogemea upande wa Ruto. Mahusiano kati yake na rais Uhuru Kenyatta yanaonekana kuingia doa baada ya Ruto kusema atagombea kiti cha urais, kwenye uchaguzi mkuu ujao, ama rais amuunge mkono au asimuunge.

Sababu za kutokuelewana kwa Rais Kenyatta na Ruto

Tangu Rais Kenyatta na kiongozi wa chama cha Orange Democratic Movement, Raila Odinga kufanya mwafaka tarehe tisa Machi, mwaka 2018, mahusiano kati ya Kenyatta na Ruto yamekuwa yakididimia.

Mara kadhaa Ruto amekosa kualikwa kwenye mikutano ya baraza la mawaziri na shughuli nyingine za serikali kama vile kuhusishwa kwenye kamati ya kukabiliana na virusi vya Korona.

Felix Ochieng ni mtaalamu wa masuala ya siasa anasema uhusiano kati ya rais na makamu wake ulikuwa wa nazi kukutania chunguni.

Hata hivyo Ruto alikosa kumlimbikizia lawama bosi wake ambaye pia ni rais akisema kuwa siku zote kiongozi yu sahihi hata baada ya Rais kumchagua Waziri wa Usalama wa Taifa Dokta Fred Matiangi kuchukua baadhi ya majukumu yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles