23.9 C
Dar es Salaam
Saturday, September 21, 2024

Contact us: [email protected]

Kampuni ya CCCC yasherehekea tamasha la Mid – Autumn ikijivunia ufanisi katika miradi

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Kampuni ya Ujenzi na Mawasiliano ya China (CCC) imeungana na raia wengine wa nchi hiyo katika mataifa mbalimbali duniani kusherehekea sikukuu muhimu ya jadi ya Wachina (Mid – Autumn) huku ikisema itahakikisha miradi inayojenga nchini inakuwa na ufanisi.

Tamasha la Mid – Autumn huadhimishwa tarehe 15 siku ya nane ya mwezi katika kalenda ya mwandamo ya Kichina ambayo ni Septemba au Oktoba kusherehekea sikukuu ya jadi ya Wachina ambayo ni muhimu zaidi ya mwaka wa China.

Septemba 16,2024 Kampuni ya CCCC imesherehekea siku hiyo muhimu kwa kuwakutanisha wadau wake zikiwemo taasisi za Serikali inazoshirikiana nazo na wananchi wanaowazunguka.

Katika tamasha hilo kulikuwa na shughuli mbalimbali za utamaduni wa nchi hiyo ambapo washiriki walionyesha umahiri katika kutengeneza vyakula, sanaa za mikono na michezo mingine.

Kampuni hiyo pia inajenga miundombinu ya mradi wa mwendokasi ambapo Ofisa Mipango ya Usafirishaji DART, Nason Bwatuta, amesema CCCC inajenga Kituo cha Kivukoni, Karakana ya Simu 2000 na eneo la Mbuyuni ambalo watakabidhiwa hivi karibuni.

“Mradi huu una manufaa makubwa kwa taifa letu na sisi pia tunapata uzoefu wa namna wanavyoendesha shughuli zao za ujenzi,” amesema Bwatuta.

Kwa upande wake BRT Contractor’s Rep

resentative, Gou Xudong, amesema tamasha hilo ni muhimu kwa nchi hiyo ndiyo maana wameungana na Wachina wengine katika sehemu mbalimbali duniani kusherehekea.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mzimuni Kawe, Raiya Nassoro, amesema; “Kampuni ya CCCC tumeshirikiana nayo kwenye mambo mengi, wamekuwa wakitusaidia katika shule zetu za Kawe A na Kawe B kwa kutupatia vifaa vya kujifunzia na mahitaji mengine ya kibinadamu kwa ajili ya watoto wenye ulemavu.

“Tunapotaka kutengeneza barabara huwa wanatusaidia greda na sisi tunachangia mafuta kwahiyo wamekuwa wako karibu na sisi wakati wote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles