25.5 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

Kamati ya Bunge ya Ardhi yampongeza Rais Samia

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Timotheo Mzava wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuanzisha Mfumo wa Unganishi wa Teknolojia ya Usimamizi wa Sekta ya Ardhi.

Pongezi hizo zimetolewa wakati wa ziara ya kamati hiyo iliyotembelea timu ya wataalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) inayoandaa mfumo huo jijini Arusha iliyofanyika Januari 8, 2024.

Mzava ameipongeza Wizara ya Ardhi kwa kazi kubwa na nzuri na kueleza kuwa kazi hiyo inakwenda kuacha alama kwa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan katika kipindi chake cha uongozi kwa kuiacha sekta ya ardhi katika mifumo bora.

“Nichukue fursa hii kumpongeza Mhe Rais kwa kazi hii nzuri, kama kamati wameridhishwa na kazi na hongereni sana na mfumo huu uende ukawe bora na kutoa huduma kwa watanzania,” alisema Mzava.

Baadhi ya wabunge wamesema mfumo huo siyo tu utarahisisha na kuharakisha huduma za sekta ya ardhi bali utajibu maswali mengi yakiwemo ya kijamii.

“Niipongeze wizara ya ardhi kwa kufanyia kazi mfumo utakaojibu maswali mengi ya kijamii na ningetamani mfumo huu ungejibu maswali na changamoto za kiuchumi,” alisema Lucy Mayenga mbunge wa viti Maalum.

Mbunge wa Makete mkoani Njombe, Festo Sanga aliipongeza Wizara kwa kuboresha mfumo na kueleza kuwa uboreshaji huo umechelewa ingawa uko katika hatua nzuri.

Hata hivyo, mbunge huyo wa Makete alitaka kufahamu utayari wa wizara ya Ardhi katika kutumia mfumo hususan kwenye eneo la usalama wa mifumo.

Naye, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amesema mfumo huu unganishi wa usimamizi wa sekta ya ardhi utarahisisha utowaji wa huduma za sekta ya ardhi kwa mtandao bila kufika ofisi za Ardhi na unatarajiwa kuanza katika mikoa mitano ya Arusha, Dodoma, Mwanza, Mbeya na Tanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles