30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Judo Tanzania Bara waahidi kurejesha ushindi nyumbani

Na Victoria Godfrey, Dar es Salaam

Uongozi wa Chama cha Judo Tanzania (JATA) umeahidi kupambana kiushindani kurejea na ushindi nyumbani katika mashindano ya Afrika Mashariki yatakayoanza Jumamosi na Jumapili visiwani Zanzibar.

Timu ya Judo Tanzania Bara inatarajia kuondoka kesho Dar es Salaam kuelekea Zanzibar.

Akizungumza na www.mtanzania.co.tz Katibu Mkuu wa JATA, Innocent Malya, amesema wachezaji wana ari na morali kutokana na wamefanya mazoezi ya nguvu.

“Kikubwa watuombee tumalize mashindano salama na pili tunawaahidi kupambana kiushindani kurejesha ushindi nyumbani kwakuwa tumejiandaa vya kutosha,” amesema Malya.

Amesema kuwa wachezaji watakaopata medali za dhahabu wa Tanzania Bara na Zanzibar wataunda timu ya Taifa itakayoshiriki mashindano ya Ubingwa wa Afrika yatakayofanyika Mei mwaka huu nchini Morocco .

Mashindano hayo ni kusaka tiketi ya kufuzu kushiriki Michezo ya Olimpiki mwaka huu Tokyo, nchini Japan.

Kwa upande wake Katibu Msaidizi wa Afrika Mashariki wa Judo Kanda ya tano, Mohamed Khamis Juma ,amesema maandalizi yamekamilika .

Mashindano ya Afrika Mashariki yatashirikisha timu kutoka Kenya,Burundi Uganda, Tanzania Bara na wenyeji Zanzibar.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles