27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Jokate ataka kuwepo askari Mzinga

Neema Paul, TUDARCo

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo amemwagiza Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi Mbagala, SSP Joseph Mwakabonga kuwataka askari wa usalama barabarani kuwepo eneo la Mzinga Kongowe kwenye shule tatu za msingi ambazo wanafunzi wengi wamekuwa wakigongwa na magari wakati wa kuvuka barabara.

Jokate ametoa maagizo hayo leo Septemba 7, alipotembelea eneo la Mzinga kufuatilia agizo lake la kujengwa matuta na alama za barabarani katika barabara ya Kilwa inayopita katika shule hizo.

Amesema jumla ya wanafunzi wanane wagongwa na magari, hali iliyosababisha wananchi kufunga barabara wiki iliyopita kutaka hatua za haraka zichukuliwe kuokoa maisha ya watoto wanaovuka kwenda shule

Aidha Jokate ametaka hatua kali zichukuliwe kwa madereva wote ambao hawafuati sheria za vivuko vya watembea kwa miguu.

Pia ameelezea umuhimu wa wanafunzi kupewa elimu ya usalama barabarani ili wawe na uelewa zaidi juu ya matumizi ya barabara na kuepusha ajali zinazoepukika .

Naye Mkuu wa shule ya msingi Kongowe, Sabina Amoni ameishukuru serikali kupitia Mkuu wa Wilaya kwa kusema kuwa watoto hao watakua salama zaidi wakiwa wanavuka barabara hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles