26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Inter: Madrid kazi mnayo

KUELEKEA mchezo wa kesho wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, kocha wa Inter Milan, Simone Inzaghi, amesema vijana wake watafanya kila linalowezekana kuiangamiza Real Madrid.

Inzaghi amekiri kuufahamu ubora wa Madrid lakini anaamini haitakuwa rahisi kwa vigogo hao wa La Liga kuondoka na pointi tatu katika mechi hiyo itakayochezwa nchini Italia.

“Wana wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kukokota mpira na tunatakiwa kujua namna ya kushughulika nao…” amesema Inzaghi.

Aidha, Vinicius Junior ameifungia Madrid mabao manne katika mechi nne za mwanzoni mwa msimu huu wa La Liga lakini Inzaghi haonekani kumtolea macho mchezaji huyo.

“Vinicius yuko kwenye kiwango kizuri lakini hatuwezi kuishia kumtazama yeye tu. Tukifanya hivyo, tunaweza kuwasahau (Karim) Benzema, (Eden) Hazard au Rodrygo Goes,” amesisitiza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles