22.9 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Mwanaidi aonya kuhusu huduma kwa wazee

Na Mwandishi Wetu, Bukoba

SERIKALI imesema haitavumilia sababu zinazokwamisha wazee kupata huduma ya matibabu kama ilivyo katika miongozo na maelekezo ya viongozi kuhusu huduma zao.

Naibu Waziri wa Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Mwanaidi Ali Khamis amesema hayo mjini Bukoba mkoani Kagera katika ziara yake Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kagera kukagua ya utoaji wa huduma kwa wazee, wanawake na watoto.

Amesema kuwa maelezo kuhusu baadhi ya dawa kuacha kutolewa kwa wazee kutokana na maelekezo ya Bima ya Afya yanahitaji kutafutiwa ufumbuzi wa kudumu ili waweze kupata huduma kama ilivyoelekezwa.

“Nimeambiwa kwamba baadhi ya dawa hazipatikani kwa wazee kwa maelekezo kadhaa kulingana na viwango na uwezo wa hospitali tusingependa kusikia baadhi ya wazee wanakosa dawa kwa sababu yoyote,” amesema

Mwanaidi amemuelekeza Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera, kuwasilisha taarifa ya upatikanaji wa dawa wizarani ili kuhakikisha wazee na makundi mengine ya kipaumbele yanapata huduma stahiki.

Katika hatua nyingine, Mwanaidi ametembelea wodi ya watoto, wajawazito na wazazi na kupata maelezo ya huduma zinazotolewa hospitalini hapo.

Aidha amewapongeza watoa huduma katika Hospitali ya Mkoa wa Kagera kwa kazi kubwa wanayoifanya na kuongeza kwamba kazi hiyo ni ya wito hivyo waendelee kujitoa na kufanya kazi kwa moyo.

Wakati huo huo, Mwanaidi ametembelea makazi ya wazee wasiojiweza ya Kiilima nje kidogo ya Manispaa ya Bukoba na kuiagiza wizara kuendelea kutoa huduma kwa wazee hao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles