33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Hatimaye Nondo aachiwa huru

NA RAYMOND MINJA IRINGA

Mahakama Kuu ya  Iringa  imemuachia huru aliyekuwa Mwenyekiti wa
Mtandao wa Wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania(TSNP), Abduli Nondo
baada ya Jamhuri kushindwa kuthibitisha maelezo iliyoyatoa  juu ya
mshitakiwa huyo.

Nondo, alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Machi
mwaka huu akikabiliwa na mashtaka mawili ya kutoa taarifa ya uongo kwa Ofisa wa polisi wa kituo cha polisi Mafinga akidai alitekwa na watu wasiojulikana na shtaka la pili alidaiwa kutoa taarifa za uongo mtandaoni.

Akitoa maelezo hayo leo Jumatatu Novemba 5, kabla ya kutoa uamuzi huo Hakimu mfawidhi wa mahakama ya Iringa, Liad Chamshama amesema Jamhuri imeshindwa kueleza kuwa mshitakiwa
alitokaje Mafinga na kwa usafiri gani hivyo mahakama imekosa ushahidi.

Chamshama amesema kuwa mahakama imekosa ushahidi kutoka upande wa Jamhuri wa kuwa mshitakiwa alikuwa wapi wakati wa tukio, hivyo mashahidi wa Jamhuri wametoa ushahidi wa hisia kwa kuwa tu simu yake ilikuwa ikitumika bila kujua aliyekuwa anaitumia.

Amesema upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha uongo wa mshatikiwa na hata kielelezo ilichopeleka mahakamani kimetia mashaka hivyo kutokana na mkanganyiko huo makahama imeshindwa  kuyaamini maelezo yaliyopelekwa mahakamani.

“Ifahamike siyo jukumu la mahakama kujua mshatakiwa alitekwa au hakutekwa hilo ni jukumu la polisi, Hivyo basi mahakama imeamua Abdul Nondo aachiwe huru, ” amesema.

Mara baada ya mahakama kumuachia huru Nondo alishindwa kujizuia na kuangua kilio mahakamani hapo akiwa ndani ya kizimba jambo lililomlazima hakimu kumtaka anyamaze .

Akizungumza nje ya mahakama hiyo mara baada ya kuachiwa huru Nondo amesema ameamini nguvu ya mahakama na kutenda haki katika shauri lake hivyo anaishukuru sana mahakama kwa kutenda haki.

“Jambo la msingi na muhimu sana kuwa ni kuwa siwezi kurudi nyuma licha ya machungu na madhila niliyopata ikiwemo kutimuliwa
shule, mapambano yataendelea niliamini Mungu yupo na nitashinda,” amesema Nondo.

Akizungumzia mwendendo wa kesi hiyo wakili wa Nondo, Jebra Kambole amesema wanaishukuru mahakama kwa kutenda haki na jinsi shauri hilo lilivyoendeshwa.

Aidha Kambole amesema  mara baada ya Nondo kuwa huru na kwa kuwa alikuwa anasoma atarudi chuo ili aendelee na masomo yake aliyosimama wakati wa kesi yake ilipokuwa ikiendelea.

 

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles