Halimashauri ya jiji la Arusha imetoa jumla ya Tshs milioni 624, ambazo kati ya hizo milioni 425 ni kwa ajili ya wanawake na milioni 199 kwa ajili ya vijana na hii ni awamu ya pili kwa Halmashauri kutoa mikopo kwa ajili ya vikundi mbalimbali.
Mara ya kwanza jumla ya milioni 405 zilitolewa, hivyo mpaka sasa jumla ya bilioni 1.24 zimetolewa kama mikopo kwa vikundi vya vijana na wanawake.
Mikopo hiyo ambayo ni mapato ya ndani ya Halmashauri ambayo ni zaidi ya 1bil kila mwezi,sambamba na hilo Halmashauri imetoa mafunzo maalum kwa ajili ya matumizi bora ya fedha hizo.
Kwa mujibu wa Halmashauri, bado itaendelea kutoa mikopo hiyo kwa wananchi wote wa Jiji la Arusha ambao kwa sasa wameshauriwa kuunda vikundi ili waweze kufaidika na mikopo hiyo.