28.3 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

GEORGE WEAH KUUKWAA URAIS?

MONROVIA, LIBERIA

MWANASOKA wa zamani wa timu ya taifa ya Liberia maarufu kama Lone Stars, na klabu za Monaco, AC Milan, na Chelsea George Weah huenda akakbidhiwa jukumu jipya iwapo matokeo ya uchaguzi mkuu nchini humo yatatangazwa kuwa ndiye mshindi wa kiti cha urais.

Kwa mujibu wa taarifa za duru za habari zinasema kuwa kura zinazoendelea kuhesabiwa zinaonesha nyota huyo wa zamani wa soka anaongoza kwa kura, kulingana na matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu wa nchini humo.

Mgombea anayefuatia ni makamu wa rais Joseph Boakai, ambaye anaongoza katika jimbo moja na mengine yanayosalia ameshika nafasi ya pili.

Mshindi atakayetangazwa atachukua nafasi ya mwanamke wa kwanza Afrika kuwa rais Ellen Johnson Sirleaf. Rais Ellen Johnson Sirleaf ambaye ni mshindi wa tuzo ya Nobel, anamaliza muda wake kwa mujibu wa katiba ya Liberia.

Takwimu kutoka tume ya uchaguzi NEC zinaonyesha Weah yupo mbele kwa majimbo 11 kati ya majimbo 15 japo zoezi la kuhesabu kura linaendelea.

Mshindi katika uchaguzi huo anatakiwa kupata 50 % ya kura zote ili aweze kutangazwa mshindi, na kama hakuna mgombea atakayefikisha kiwango hicho, uchaguzi wa marudio utapewa nafasi kwa muda usiozidi siku 20 yaani mnamo mwezi Novemba.

Hata hivyo duru mbili ndio zitaamua ushindi wa rais mpya wa nchi hiyo. Uchaguzi huu ni wa kihistoria ambao ambapo itakua mara ya kwanza tangu kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe utawala unakabidhiwa kwa njia ya kidemokrasia kutoka kwa rais anayemaliza muda wake akimkabidhi rais aliyechaguliwa.

Miongoni mwa wagombea katika uchaguzi huo ni Joseph Nyumah Boakai, Charles Brumskine, Alexander Cummings, Benoni Urey na George Weah.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles